Mwanamume mwenye umri wa miaka 74 kutoka Maragua, Kaunti ya Murang’a, nchini Kenya ambaye alitamba mitandaoni baada ya kujichimbia kaburi sasa amenunua jeneza ambalo litatumika kumzika.
Samuel Karanja maarufu kama Kumenya aliwatembelea mmoja wa maseremala mjini Murang'a ambapo aliagiza aundiwe jeneza kulingana na muundo alioutaka kwa mujibu wa ripoti ya K34 Digital.
Jeneza hilo lina jina lake na rangi ya kijivu ya kipekee ambayo sio kawaida kwenye soko la kuuza majeneza.
Karanja alisema mara baada ya fundi kumaliza kumuundia jeneza atalipeleka kwake na kulihifadhi katika kaburi alilojijengea awali.
Alisema atalihifadhi jeneza hizo vizuri akisubiri safari yake ya mwisho duniani.
Karanja aliandaa sehemu yake ya kupumzika mnamo Jumanne, Januari 12, 2021 na pia alitayarisha wasifu wake ambao alisema utasomwa wakati wa ibada ya mazishi yake.
Alisema aliiandaa tanzia hiyo kwa sababu ni yeye tu anajielewa kumliko mtu mwingine yeyote.
"Sitaki watu watatizike wakati wa mazishi yangu, watu wengi huwafanya jamaa zao kuhangaika wanapoaga dunia lakini sitaki familia yangu ipitia hilo," alisema.
Karanja alifichua kwamba tayari ameratibu jinsi atakavyozikwa ambapo kaburi lake halitawekwa maua, msalaba na kaburi lake lisifunkiwe kwa mchanga.
Hata hivyo hatua yake iliwaacha wengi vinywa wazi huku mkewe Jane Wanjiru akisema hakubaliani na matayarisho ya mumewe.
Mzee huyo alipuzilia mbali tofauti alizokuwa nazo mkewe kuhusuhatua yake na kusema kwamba ni vyema kila mmoja ajitayarishe kwa safari yake ya mwisho ili kuzuia mizozo ya familia wakati jamaa wao anapoaga dunia.
Chanzo- Tuko News
Social Plugin