Jamaa ambaye alimtusi mama yake mzazi amekutwa na hatia na kisha kutozwa faini ya KSh 10,000 sawa na shilingi laki mbili za Kitanzania.
Iwapo mshtakiwa, David Maloba Omar atashindwa kulipa hela hizo basi atalazimika kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani kwa kuvuruga utulivu.
Kwa mujibu wa Nairobi News, mahakama iliarifiwaa kuwa Oduor alizua vurugu nyumbani kwake Gaudensia Oduor mtaani Lang'ata mwezi Juni 18.
Mshukiwa alisemekana kumtusi, kumhangaisha na kutishia kumtandika mamaake nyumbani kwake mtaani Langa'ta
Mshtakiwa huyo alisomewa adhabu yake na hakimu Charles Mwaniki katika mahakama ya Kibera baada ya kukiri mashtaka. Mahakama aidha iiliarifiwa kuwa Oduor alitishia kumtandika mamake.
Mamaake alilazimika kujifungia ndani ya nyumba akihofia maisha yake. Alirejea kosa hilo siku iliyofuata na kisha akaelekea jikoni kupika baada ya mamake kujifungia ndani ya chumba chake cha kulala. Alilazimika kumshtaki kwa polisi.
Uchunguzi wa polisi ulionyesha kuwa mwaka jana mama huyo alilalamika kuhusu tabia ya mwanawe. Kupitia wakili wake, aliiambia mahakama kuwa amesuluhisha suala hilo na kusameheana na mamake, alielezea majuto yake na kuomba msamaha.
Chanzo - Tuko news