Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, Miundo michundo alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula ameziomba Taasisi za Fedha zikiwemo Benki ziwakopeshe Wachimbaji Wadogo wa Madini ili wanunue Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ kutokana na wengi wao kutokuwa na mitaji ya kununua mitambo hiyo ya kuchimba na kuchenjua madini.
Kashi Salula ameyasema hayo leo Jumapili Julai 25,2021 wakati Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula amesema ni vyema taasisi za kifedha zikawapa mikopo wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kununua vifaa/mitambo kwa ajili ya uchimbaji na uchenjuaji madini ili uchimbaji wao uwe na tija.
“Kampuni yetu inajihusisha na uchimbaji na uchenjuaji wa madini lakini pia tunajihusisha na utengenezaji wa miundo michundo na kuuza nchi nzima. Tunaomba taasisi za kifedha zikiwemo Benki ziangalie namna ya kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wanunue mitambo kwa ajili ya kuchimba na kuchenjua madini”,amesema Gacha.
Katika hatua nyingine amesema wametumia fursa ya maonesho kuonesha namna wanavyofanya kazi.
Salula amesema pia kampuni yao inajihusisha na masuala ya uchomaji na ubunifu,uundaji wa mashine za nafaka ‘vinu’,ufundi wa mitambo ya viwandani,zana za mgodini na matengenezo mbalimbali.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina amempongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula kwa kazi nzuri anayofanya ya kutengeneza na kuuza Miundo Michundo nchi nzima huku akipendekeza mafundi michundo akiwemo Kashi Salula kupewa mafunzo zaidi ya kuboresha kazi yao ikiwa ni pamoja na kuwapeleka nje ya nchi kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi.
Naye Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwezesha wachimbaji wadogo na kutenga maeneo ya msingi yenye taarifa ya Jiolojia na utafiti.
“Mpaka sasa kuna Masoko 39 na vituo 50 vya kuuzia madini.Serikali inaendelea kusimamia vituo hivi vya ununuzi wa madini na kufanya jitihada za kuongeza vingine.Tunawasihi watu wote wanaojihusisha na mnyororo wa madini waache kutorosha madini kwani bado kuna utoroshaji wa madini, hasara watakayopata wakikamatwa wakitorosha madini ni kubwa sana”,amesema Prof. Manya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa nne kushoto) namna wanafanya kazi alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika Uwanja wa Zainab Telack katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga leo Jumapili Julai 25,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, Miundo michundo alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akizungumza wakati Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, Miundo michundo alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula akiziomba Taasisi za Fedha zikiwemo Benki ziwakopeshe Wachimbaji Wadogo wa Madini ili wanunue Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ wakati Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya alipotembelea banda la Shinyanga Best Iron kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) akizungumza kwenye banda la Shinyanga Best Iron katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Miundo Michundo ‘Pembejeo za uchimbaji’ katika banda la Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog