Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA FAMILIA YA AJABU YA WATU 9, WOTE WAMEZALIWA TAREHE MOJA



Mwalimu mmoja nchini Pakistan kwa jina Amir Ali, amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na familia yenye watu wengi waliozaliwa katika tarehe moja –ya Agost mosi baada ya watu tisa wa familia moja kuzaliwa tarehe hiyo.

Rekodi ya awali ilikuwa imeshikiliwa na familia kutoka Caymans kwa miaka tisa ambapo watoto watano walikuwa wamezaliwa tarehe 5 mwezi Februari lakini miaka tofauti.

Amir, mkazi wa Larakana , alisema alizaliwa tarehe 1 mwezi Agosti ,Mke wake alizaliwa tarehe moja mwezi Agosti , Binti yake wa kwanza Sindh alizaliwa mwanawe wa kiume wa pili Amber na wanae pacha Ammar na Ahmar, wote walizaliwa tarehe 1 Agosti.

Amir Ali anaamini katika elimu ya nyota- nyota yake ni Asad au Zmarai na inaelezwa kuwa namba ya kwanza ya bahati, wakati alipoanza kazi tarehe 1 mwezi Agosti na kuoa tarehe 1 mwezi Agosti.

Amir anasema familia yake yote inasheherekea siku ya kuzaliwa kwao siku moja. Bw. Amir pia anaamini katika unajimu na kuandika ushairi. Ana shahada ya uzamili kwenye masomo kadhaa, ikiwemo sayansi ya jamii, mahusiano ya kimataifa na uchumi.

Tarehe 1 mwezi Agosti, familia yote husheherekea kwa pamoja, Bw. Amiri anasema. Anaongeza kuwa watoto wote wamezaliwa nyumbani kisha wakasajiliwa na mamlaka za manispaa. Aliongeza kuwa kwa ushauri wa rafiki yake, alituma maombi ya usajili kwa ajili ya kuwekwa rekodi kwenye Guiness Book of World Records.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com