Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Meneja Mahusiano Serikali na Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Bi. Vivian Nkhangaa (kulia) wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB katika shule ya Msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya NMB imetoa msaada wa mabati 468 yenye thamani ya shilingi Milioni 15.4 kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Lyabusalu, Ishololo na shule ya Sekondari Imenya pamoja na madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa ajili ya shule ya msingi Mwenge katika wilaya ya Shinyanga.
Akikabidhi mabati na madawati hayo leo Alhamis Julai 29,2021 kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse amesema wametoa msaada huo ili kuboresha sekta ya elimu katika wilaya ya Shinyanga ikiwa ni kipaumbele cha Benki ya NMB kwenye sekta ya elimu na afya.
“Leo tumekabidhi mabati 468 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambazo ni shule ya Sekondari Imenya, shule ya msingi Ishololo na shule ya msingi Lyabusalu ambazo kila shule imepata madawati 156 yenye thamani ya shilingi 15.4. Lakini pia tumekabidhi madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga na kufanya jumla kuwa shilingi Milioni 18.4”,ameeleza Magesse.
Amesema Benki ya NMB itaendelea kusaidia kwenye maeneo yenye changamoto na kuendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake katika kuhakikisha inatatua changamoto katika sekta ya elimu na afya.
“Kama taifa lina watu wenye elimu n afya wataweza kushiriki katika shughuli za maendeleo. Ndiyo maana sisi NMB tumejikita kwenye elimu na afya. Kupitia jamii ndiko wateja wao wanapotoka hivyo umekuwa utamaduni wetu kurudisha kwa jamii faida tunayopata”, ameongeza.
Magesse ametumia fursa hiyo kuwaomba watu wote waliofaidika na Benki ya NMB pamoja na wananchi kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo huku akiwashauri wananchi kujiunga na bima mbalimbali zinazotolewa katika benki ya NMB, mikopo kwa wakulima, watumishi , wafanyabiashara, wajasiriamali na wafugaji.
Akipokea mabati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameipongeza Benki ya NMB kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa ili kuboresha sekta ya elimu na afya.
“Benki ya NMB mmekuwa mkitusaidia mara kwa mara, mmekuwa mkijitokeza kila mara kwa mara. Kwa kweli tunajivunia sana uwepo wa Benki hii. Msaada huu mliokabidhi niliwaomba mzisaidie shule hizi na kweli leo mmetimiza ahadi yenu. Tunawashukuru sana na tunaomba msichoke kuzisaidia shule zetu kwani bado mahitaji ni mengi”,amesema Mboneko.
Mboneko amesema serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya NMB muda wowote huku akiwasihi wananchi kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Benki ya NMB ambao sasa wanataka kufungua Tawi lao katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga eneo la Iselamagazi.
Mkuu huyo wa wilaya amezitaka shule zilizopata msaada huo kutunza miundo mbinu ya shule huku akiwataka wazazi na walezi kutowakatisha masomo watoto wao kwa kuwaozesha kwani inakatisha ndoto za watoto.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kwamba msaada huo utachangia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yaliyotolewa na Benki ya NMB leo Alhamisi Julai 29,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yaliyotolewa na Benki ya NMB leo Alhamisi Julai 29,2021.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021. Amesema ni mara ya pili sasa Benki ya NMB inatoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Makabidhiano ya mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Imenya na shule ya Msingi Ishololo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yaliyotolewa na Benki ya NMB.
Muonekano wa jengo la madarasa mawili katika shule ya Sekondari Imenya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambalo litaezekwa kwa mabati yaliyotolewa na Benki ya NMB.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Manonga, Sebastian Kayaga akizungumza wakati Benki hiyo ikikabidhi madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Ester Makune akiishukuru Benki ya NMB kutoa msaada wa madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiishukuru Benki ya NMB kutoa msaada wa madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Zoezi la makabidhiano ya madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati), Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse na viongozi mbalimbali wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB katika shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la makabidhiano ya madawati 50 katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga likiendelea
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akiishukuru Benki ya NMB kutoa mabati 156 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Alhamisi Julai 29,2021.
Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ukiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiishukuru Benki ya NMB kutoa mabati kwa ajili ya ujenzi madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (katikati) akimkabidhi mabati Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa tatu kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Zoezi la makabidhiano ya mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea
Zoezi la makabidhiano ya mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea
Wanafunzi wa shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanayoendelea.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga akiishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwahamasisha wanafunzi wa shule ya msingi Lyabusalu iliyopo katika kata ya Lyabusalu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin