Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AUAWA BAADA YA KUMFUMANIA LIVE MAMA YAKE 'AKICHEPUKA' NA MWANAUME MWINGINE KWAO


Kijana aliyejulikana kwa jina la Budagala Vita (29) mkazi wa kijiji cha Bokondo, Tarafa ya Butundwe, Wilaya ya Geita  ameuwa kwa kucharangwa mapanga baada ya kumfumania mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanaume mwingine wakati baba yake mzazi akiwa safarini.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea Juni 28, 2021 katika kijiji cha Bokondo, Tarafa ya Butundwe, Wilaya ya Geita ambapo Budagala aliuawa kwa kukatwa na mapanga shingoni na watu wasiojulikana.

"Kijana huyo aliuawa kwa kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana baada ya kumkuta mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanaume mwingine wakati baba yake mzazi Vita Bupilipili akiwa safarini mkoani Kagera kwenda kutafuta maisha Juni 26,2021 na kumuacha mke wake pamoja na mtoto wake huyo",amesema Kamanda Mwaibambe.

Ameeleza kuwa Budagala alimkuta mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanaume mwingine nyumbani kwao na kusababisha mgogoro ndani ya familia hiyo na baada ya tukio hilo mama mzazi wa marehemu alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Amesema Jeshi la polisi inawashikilia watu watano kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo na mama mzazi anatafutwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com