Na Dinna Maningo,Tarime
TIMU ya Mpira wa Miguu ya West Ham United Sirari maarufu wapiga nyundo ambao ni mafundi waezekaji wa mabati kwenye nyumba wameichapa mabao matatu kwa moja wapinzani wao timu ya Stand F.C Ng'ereng'ere zote zikiwa zinatoka wilayani Tarime mkoa wa Mara.
Mchezo huo ulifanyika jana katika uwanja wa Tarafa Sirari wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Ujirani Mwema Mapesa Cup uliozinduliwa na Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa.
Mchezaji wa timu ya wapiga nyundo Musa Samwel (Benzema) alitandika gori la kwanza dakika ya 8 tangu kuanza kwa mchezo huo majira ya saa 10:35 jioni ,timu hiyo iliwakimbiza mchakamchaka kwa kuwacharanga bao jingine la pili dakika ya 20 ya mchezo lililofungwa na Nick Nicolous hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo kwa dakika 45,timu ya wapiga nyundo waliibuka na magori 2 huku Stend F.C ikiambulia patupu.
Katika kipindi cha pili cha mchezo timu ya wapiga nyundo ilifunga bao jingine la 3 dakika ya 75 lililofungwa na George Suguta, nao Stend F.C wakaamua kujifuta machozi ambapo mchezaji Dibro Chacha kwa kufunga goli 1,huku wachezaji wawili wa Stend F.C Patrick William na Emanuel Bwire wakionywa kwa kadi ya njano.
Hadi mchezo unakwisha dakika ya 90 timu ya West Ham maarufu Wapiga nyundo iliibuka kidedea kwa ushindi kwa kuichapa mabao 3 huku Stend F.C wakiambulia bao 1.
Akizindua mashindano hayo mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano ya Ujirani Mwema Mapesa Cup Victoria Mapesa alisema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuibua vipaji kwa vijana katika soka.
"Nimeanzisha mashindano kwasababu michenzo ni sehemu mazoezi ya kujenga afya,kujenga mahusiano kwa vijana kupitia michezo,Vijana kuendeleza vipaji vyao na tumeshuhudia wameanza vizuri na watazamaji wamehudhulia wengi hii inaonyesha kuwa Tarime wanapenda michezo",alisema Mapesa.
Mapesa aliwaomba wachezaji kucheza vizuri huku akiahidi kutoa zawadi kwa washindi siku ya fainali julai 31 na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuwashangilia wachezaji katika kipindi chote cha mashindano hayo.
Diwani wa viti maalumu Josephine Hombe aliwapongeza vijana kwa mchezo "Vijana wamejitahidi kuna vipaji wakisaidiwa watafika mbali,refa wa timu ya stend ajitahidi kuwafundisha wachezaji kwenye mechi ya jana mpira ukielekea mahali wote wanalundikana sehemu moja wamepoteza magori mengi,hakuna beki anayebaki kumsaidia kipa kwasababu wote wanarundikana sehemu moja badala yakutawanyika kwenye uwanja",alisema Hombe.
Diwani wa kata ya Gwitiryo Nashon Mchuma aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuziwezesha timu za mpira kimchezo huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Sirari Joel Mwita akimpongeza Diwani Mapesa kwa kuanzisha mashindano ya ujirani mwema licha yakwamba ni mwanamke lakini anaunga mkono mpira wa miguu.
Msimamizi wa mashindano hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya ujirani mwema Mapesa Cup Mallison Harun alisema kuwa timu 16 zitashiriki mashindano hayo ya mpira wa miguu ambazo zitacheza kwa makundi.
"Kundi la A ni kati ya timu ya West Ham United ya Sirari na Stend F.C Ng'ereng'ere kutoka kata ya Regicheri ,kundi B ni Magena FC kutoka kata ya Nkende na Tarime United,kundi C timu ya Talent Sport na Nyabisaga F.C, kundi D ni Home boys F.C Sirari na Remagwe F.C,kundi E ni timu ya Madereva FC Sirari na Sirari Youngs.
Zingine ni kundi F ambayo ni timu ya Tarime TC ambao ni muungano wa waajiriwa wa serikali ndani ya halmashauri ya mji Tarime na Nyabitocho F.C kata ya Mbogi,kundi la G ni Sang'ang'a F.C kutoka kata ya Pemba na Forodhani FC kutoka kata ya Sirari,kundi H ni timu ya Buriba F.C Sirari na Amani F.C ambayo ni timu ya mafundi ujenzi kutoka Sirari.
Harun alisema kuwa pamoja na mashindano hayo kuna changamoto mbalimbali ikiwemo ya washiriki wa mpira kutoelewa sheria za uchezaji wa mpira na maamuzi yanapofanyika huona kama wameonewa.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo baadhi ya wachezaji na mashabiki walikuwa na haya yakusema,Boniphace Chacha mchezaji wa timu ya West Ham United alijigamba akisema "sisi ndiyo wapiga nyundo timu imara lazima tuwaumize wakajipange vizuri tutacheza vizuri na kombe tunachukua",alisema.
Mchezaji wa timu ya Stend Ng'ereng'ere Gidion Mwita alisema "Tumefanya vibaya wachezaji wengi waliingia mchezoni wakiwa wamepaniki, viungo namba 6 na 8 wametuangusha sana tunaenda kujipanga upya "alisema.
Shabiki wa timu ya wapiga nyundo Zabron Marwa alisema "Vijana wamejitahidi sana jinsi walivyochapa mabao ndivyo hivyohivyo walivyo kwenye ubora wa kuezeka mabati ni wataalamu sana wa kugongelea mabati na ndiyo maana umeona wamewachapa mabao 3 timu ya Stend ",alisema.
Muamuzi namba 4 Amos Sabai alisema kuwa mazingira ya uwanja si rafiki kwa michezo hivyo anawaomba wadau kujitokeza kuboresha uwanja ili uwe rafiki kwa wachezaji.
Diwani wa viti maalumu na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Victoria Mapesa akipiga mpira wakati akizindua mashindano ya ujirani mwema Mapesa Cup
Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya West Ham United maarufu wapiga nyundo kutoka kata ya Sirari
Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya West Ham United maarufu wapiga nyundo kutoka kata ya Sirari
Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Stend FC Ng'ereng'ere ya kata ya Regicheri
Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Stend FC Ng'ereng'ere ya kata ya Regicheri
Diwani wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime, aliyekuwa mgeni rasmi na mdhamini wa mashindano hayo Victoria Mapesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Stend FC Ng'ereng'ere ya kata ya Regicheri
Social Plugin