Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza na kutaja shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 72.
Msonde amesema Kemebos ya Kagera yenye watahiniwa 35 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Dareda ya Manyara watahiniwa 101.
Nafasi ya nne imechukuliwa na Tabora Girls yenye watahiniwa 100 ikifuatiwa na Tabora Boys yenye watahiniwa 120.
Nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na watahiniwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye watahiniwa 53.
Zakia Meghji imeshika nafasi ya nane ikitokea mkoani Geita. Ilikuwa na watahiniwa 31, ikifuatiwa na Kilosa ya Morogoro yenye watahiniwa 91, na Mzumbe watahiniwa 135.