Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kindi wilayani ya Moshi mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kumuua mama yake mzazi Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kumng’oa macho.
Taarifa imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linaelezwa kuwa limechangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda, amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 katika eneo la Kibosho Sambarai.
Via Nipashe
Social Plugin