Mchango huu pia hutumika kama mpango wa uhamasishaji kwa umma juu ya umuhimu wa kufuata matibabu ili kuhakikisha wenye matatizo wanapona na kuzuia ulemavu.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika CCBRT, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema: "Mchango wetu unathibitisha zaidi kujitolea kwetu kusaidia jamii zinazotuzunguka. Matibabu ya miguu pinde nchini ni mada ambayo inahitaji utangazaji na kama kampuni ya simu inayoheshimika, tuko hapa leo kubadili hadithi, tunahitaji ushiriki wa jamii na nguvu ya kuhakikisha kwamba kila mtoto aliye na miguu pinde Tanzania, anapata matibabu bora na kwa wakati kwa kutumia njia ya Ponseti, kama matibabu ya kiwango cha juu na hivyo kuwapa fursa sawa ya kuishi maisha yenye tija kama walivyo wengine,".
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi, aliishukuru Tigo kutokana na msaada huo endelevu ambao umekuwa ukisaidia kuokoa maisha ya watoto wengi Watanzania.
“Tigo Tanzania imeonyesha mfano kwa jukumu muhimu ambalo sekta binafsi imeamua kulichukua katika kuhakikisha inapunguza na kutatua shida za jamii.
“CCBRT, kwa miaka mingi imeweza kushughulikia moja ya mambo magumu zaidi ya matibabu ya miguu pinde, kuhakikisha matibabu yanakuwa endelevu na ufuatiliaji, kupitia uvumbuzi na msaada wa Tigo, kuna jukwaa la kukumbushana kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS), la CCBRT linaweza kutuma njia ya simu za mkononi kukuza ufuatiliaji ili wagonjwa watibiwe kikamilifu, bila athari yoyote.
“Kwa hivyo ningependa kuwahimiza sekta binafsi kuendelea kutupatia misaada ili kuhakikisha tunatokomeza tatizo hili na kulimaliza kabisa,” alisema.
Miaka mitatu iliyopita ya ushirikiano huu imeshuhudia karibu kesi 1,500 mpya za miguu pinde kwa watoto, wanaofaidika na matibabu ya miguu yanayobadilisha maisha kwa njia ya Ponset na mamia wamefanyiwa upasuaji CCBRT.
Katika miaka ya hivi karibuni, kesi hizo zimezidu kupungua na kwamba CCBRT inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kwa ajili ya kuhakikisha wanafikia malengo.
Social Plugin