RC SENGATI AKUTANA NA WADAU KUPANGA MIKAKATI YA KUZUIA MAJANGA YA MOTO SHULENI....POLISI, ZIMAMOTO WATOBOA SIRI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati ameongoza kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto yanayotokea katika taasisi na shule mbalimbali.

Kikao hicho kimefanyika leo Ijumaa Julai 16,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Maafisa Elimu, Skauti,Waandishi wa Habari n.k ambao kwa pamoja wamekubaliana kushiriki kikamilifu katika kuzuia vyanzo vinavyosababisha kutokea kwa majanga ya moto.

Mkuu huyo wa mkoa amesema ni jukumu la kila mtu katika jamii kushiriki kuzuia vyanzo vinavyosababisha majanga ya moto kwani yanakinzana na suala la amani.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwani tumekuwa tukisikia majanga ya moto katika mikoa mingine hivyo ni vyema tupange mikakati ya kuzuia majanga ili kuwa salama na kuwa na amani kwani majanga yanapotokea yanarudisha nyuma maendeleo",amesema Dkt. Sengati.

“Njia mojawapo ya kudhibiti majanga ya moto kwenye shule zetu hasa hizi za bweni ni kuwa na ulinzi shirikishi, kila shule iwe na Walimu walezi (Matron au Patron),kufanya ukaguzi wa mara kwa amara kwa wanafunzi ili kubaini kama wana vitu vinavyohatarisha usalama pamoja na kusuluhisha Migogoro ya ndani na nje ya shule”,amesema Dkt. Sengati.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP George Kyando ameitaja mikakati inayopendekezwa na Jeshi la polisi ili kuzuia majanga ya moto katika taasisi na shule kuwa ni pamoja kila shule na taasisi iwe na walinzi makini , wale waliopitia mafunzo ya ulinzi.

Pendekezo jingine ni pamoja na shule za bweni ziwe na ulinzi shirikishi, kila shule iwe na Matron au Patroni ili kuhakikisha wanafuatilia wanafunzi wanaokuwa mabwenini na kwamba ni vizuri shule iwe na fensi/uzio, geti ili kila anayeingia pale ajulikane, ahojiwe, anaingia kufanya nini.

Kamanda Kyando pia ameshauri pia viwepo vifaa vya awali vya kuzimia moto, mfano mchanga, Fire extinguisher na pia watu wapate mafunzo ya kutumia hivyo vifaa.

“Mienendo ya wanafunzi ifuatiliwe, Itikadi za wanafunzi zifuatiliwe mfano kujiingiza katika siasa au itikadi kali ili kuepuka vishawishi. Wanafunzi wakaguliwe mara kwa mara ili kubaini kama wana pasi za umeme,heater,viberiti, taa za kandili. Wasiwe na vitu visivyofaa kuwa navyo shuleni”,ameongeza Kamanda Kyando.

Kamanda Kyando amesema pia ni lazima migogoro ya ndani na nje ya shule itatuliwe mapema sanjari na utoaji elimu ya namna ya kujikinga na majanga ya moto itolewe kwa wanafunzi.

“Majengo mengi ya shule zetu na miundo mbinu yake imechakaa,hivyo ni vizuri maeneo ya shule yakaguliwe na Tanesco, nyaya ziangaliwe. Milango ya shule iwe ya kufungulia nje/kusukuma kwa nje, na madirisha yasiwekewe nondo”,ameeleza.

Kwa Upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, Inspekta Edward Lukuba amesema jeshi hilo lina wajibu wa kuzima moto na kutoa elimu ya namna ya kuzuia majanga ya moto akisema wanaendelea kutoa elimu katika shule na taasisi mbalimbali.

“Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikichangia kutokea kwa majanga ya moto, zipo hujuma lakini mifumo ya umeme inakuwa imechakaa, hitilafu ya umeme,migogoro shuleni,mifumo mibovu ya umeme ‘Wiring’ na mfumo mbovu wa majengo”,amesema Inspekta Lukuba.

“Ili kudhibiti majanga ya moto yanayotokana na sababu za kibinadamu ni Lazima tuboreshe hii mifumo ya umeme, tuwatumie mafundi kutoka TANESCO na ni vyema tuweke sera za usalama shuleni, Wakurugenzi wa halmashauri waajiri fire manager, wafanye risk assessment,tuwe na vifaa vya kuzimia moto na kuifanyia service,tuwe na Smoke detector, gas detector na fire water reserve”,ameongeza Inspekta Lukuba.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati akizungumza wakati akifungu kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga kilichofanyika leo Ijumaa Julai 16,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto.
Kamanda wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Inspekta Edward Lukuba akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti majanga ya moto kwenye taasisi na shule mkoani Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post