Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AKUTANA NA MWANAE WA MIAKA 24 BAADA YA KUIBIWA


Mtu mmoja nchini China amekutana na mtoto wake wa kiume baada ya miaka 24 akimsaka ambapo alisafiri mwendo wa kilomita 500,000 (maili 310,000 ) kwa pikipiki kote nchini.

Guo Gangtang alipokonywa mtoto wake huyo wa kiume na watu wawili wanaofanya biashara haramu ya binadamu alipokuwa mbele ya nyumba yao katika jimbo la Shandong.

Kutoweka kwa mwanae kulipelekea kutengenezwa kwa filamu mwaka 2015, ambayo ilichezwa na mchezaji filamu nyota wa Hong Kong Andy Lau.

Kutekwa nyara kwa watoto ni tatizo kubwa nchini Uchina, huku maelfu ya watoto wakiibiwa kila mwaka.

Kulingana na Wizara ya usalama wa umma ya Uchina, polisi waliweza kumpata mtoto huyo kwa kutumia kipimo cha vinasaba -DNA.

Washukiwa watatu walifuatiliwa na baadaye kukamatwa, limeripoti gazeti la Global Times.

Washukiwa ambao walikuwa wanachumbiana wakati huo, walikuwa wamepanga kumteka mtoto kwa lengo la kumuuza kwa ajiloi ya kuipata , imesema taarifa ya China News.

Baada ya kumpata mtoto wa Bw Guo akicheza peke yake nje ya nyumba, mshukiwa wa kike aliyetambuliwa kwa jina pekee la baba yake kama Tang , alimvuta na kumchukua hadi kwenye kituo cha basi ambako mpenzi wake, Bw Hu, alikwa akisubiri.

Wawili hao walipanda basi linalosafiri kwenye miji mbali mbali wakaelekea hadi katika jimbo jirani la Henan na kumuuza huko.

Vyombo vya habari vya jimbo hilo vinaripoti kuwa kijana huyo alipatikana akiwa bado anaishi katika jimbo hilo.

"Sasa kwasababu mtoto amepatikana, kuanzia sasa ni furaha ," Bw Guo aliwaambia waandishi wa habari.

Baada ya mtoto wake kutekwa nyara mwaka 1997, Bw Guo alirirpotiwa kusafiri katika zaidi ya majimbo 20 kote nchini Uchina nyuma ya mwendesha pikipiki akifuata taarifa alizopewa na watu za mahala anakoweza kuwa mtoto wake.

Katika mchakato huo, alivunjika mifupa katika ajali za barabarani na kukabiliana na wezi. Pikipiki 10 pia ziliharibika.

Akitembea na bango la picha ya mwanae wa kiume, anasemekana ameishi akiweka akiba kwa ajili ya kumtafuta mwanae, akilala chini ya madaraja, na kuomba pesa alipoishiwa.

Wakati akimsaka mwanae, pia amekuwa mjumbe maarugu wa mashirika ya watu waliopotea nchini Uchina, na amesaidia wazazi takriban saba kuwapata watoto wao waliotekwa nyara.

Mara taarifa kwamba mtoto wa Bw Guo amepatikana ilipotangazwa, mitandao ya habari ya kijamii ya Uchina ilifurika kwa ujumbe wa kumsifu baba huyo.

"Wazazi wengi labda hata wangelikuwa wamekata tamaa muda mrefu uliopita. Ni mtu mwema sana na nimemfurahia kusema kweli ," mtu mmoja aliandika kwenye ukumbi wa mabloga wa Weibo.

Nchini Uchina, utekeji nyara na usafirishaji haramu wa watoto wachanga umekuwa tatizo kwa miongo mingi.

CHANZO-BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com