Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna haja ya kuwakamata raia wa taifa hilo wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya.
Akizungumza na vyombo vya habari rais huyo ameshutumu wale wanaosambaza habari kwenye mitandao kwamba yeye amefariki dunia.
Amesema kwamba wale wanaohusika na habari kama hizo wanapaswa kusakwa na kukamatwa kwa kuwa wamekuwa wakipotezea watu muda wao.
Alisema: Tatizo jingine ambalo linapaswa kutatutiliwa ambalo sio la kiusalama bali la kijinga ni mitandao ya kijami. Mitandao ya kijami imekuwa ikisema kwamba museveni amefariki. Hivyobasi naitaka idara ya usalama kusuluhisha tatizo hilo.
Nataka wawafuatilie kwa haraka wale wanaozua uvumi kama huo.
Twitter Kumekuwa na uvumi katika siku za hivi karibuni kwamba kiongozi huyo alikuwa amesafirishwa kutoka nchini Uganda na kupelekwa nchini Ujerumani akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua maradhi ya tatizo la kupumua linalohusishwa na ugonjwa wa corona.
Hata hivyo akizungumza Rais Museveni alisema kwamba wale wanaozua habari kama hizo wanapaswa kufuatiliwa na vyombo vya usalama ili kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Chanzo - BBC SWAHILI
Social Plugin