Picha aliyoiweka Leina kupitia ukurasa wake wa Twitter, ikionesha yeye na Albert wakifunga ndoa
Mwanadada anayejiita Leina, ametuma ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akimtafuta mwanaume ambaye alifunga naye ndoa miaka ya nyuma wakiwa watoto.
Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa Twitter, mwanadada huyo Leina, ameweka picha ikimuonyesha yeye wakati wa utoto akiwa amefunga ndoa na mtoto mwenzake.
Leina aliweka picha hiyo juzi Juni 27, 2021, na kuandika kuwa kijana huyo anaitwa Albert na sasa hajui yuko wapi na ndoa hiyo walifunga wakiwa darasa la pili.
"It’s the bride for me, Ps: This boy’s name is Albert, i don't know where you are, but we got married in primary 2 at assembly," aliandika mwanadada huyo.
Social Plugin