Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KLABU YA MAZOEZI PJFCS YACHANGIA DAMU,MITUNGI YA OKSIJENI KUSAIDIA WENYE CHANGAMOTO YA UPUMUAJI HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS), Sadick Kibira 'Kibira Gas' akimkabidhi Mitungi ya Hewa ya Oksijeni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga imetoa msaada wa Mitungi 16 ya Hewa ya Oksijeni ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji, kufanya usafi na kuchangia damu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi ya Hewa ya Oksijeni katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 7,2021 Mwenyekiti wa PJFCS, Sadick Kibira amesema Klabu hiyo ya mazoezi imeamua kuchangishana fedha kununua mitungi ya hewa ya Oksijeni yenye thamani ya shilingi 928,000/= ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji.

"Katika kusherekea Sikukuu ya Saba Saba kila mwaka Klabu ya Mazoezi PJFCS huwa inaadhimisha mwaka wa Kimazoezi, tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali kwa wahitaji na kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu. Leo asubuhi tumefanya mazoezi katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kasha tumekuja katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kufanya usafi, kuchangia damu na kukabidhi mitungi ya hewa ya Oksijeni",amesema Kibira.

“Mitungi hii ya Hewa ya Oksijeni itasaidia kupunguza changamoto ya upumuaji kwa wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga lakini pia uchangiaji damu utasaidia kuokoa maisha kwa watu wenye uhitaji wakiwemo watu wanaopata ajali, watoto na akina mama wajawazito”,ameongeza Kibira.

Kwa upande, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum ameishukuru Klabu ya Mazoezi ya PJFCS kwa kutoa msaada huo wa mitungi ya Hewa ya Oksijeni ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji.

Naye Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul amewapongeza wanachama wa Klabu ya Mazoei ya PJFCS kwa msaada huo unaolenga kuokoa maisha ya watu akibainisha kuwa ni jambo la fadhila na baraka kusaidia wagonjwa huku akiwataka watu wengine waige mfano wa PJFCS kusaidia watu wenye uhitaji.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS), Sadick Kibira akizungumza wakati akikabidhi Mitungi ya Hewa ya Oksijeni kwa  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum (kulia) ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 7,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum akizungumza wakati wa kupokea mitungi ya hewa ya Oksijeni iliyotolewa na  Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS), Lucas Moris akizungumza wakati wakikabidhi Mitungi ya Hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS), Sadick Kibira akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum (kulia) stakabadhi ya malipo ya Mitungi ya Hewa ya Oksijeni iliyonunuliwa na PJFCS ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS), Sadick Kibira akimkabidhi Mitungi ya Hewa ya Oksijeni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum (kulia) ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakipiga picha ya kumbukumbu wakiwa na mitungi ya hewa ya Oksijeni katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakifanya usafi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakiwa katika Kituo cha Kuchangia Damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akiwashukuru na kuwapongeza Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS)  kwa kutoa msaada wa mitungi ya hewa ya Oksijeni na kuchangia damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakichangia Damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakichangia damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Awali Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakiwasili katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wakiendelea na michezo katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga

Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wapiga picha ya kumbukumbu katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga
Wanachama wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) wapiga picha ya kumbukumbu katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com