Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANUSURIKA KICHAPO AKITUMIA FEDHA ALIZOCHANGISHA 'GROUP LA WHATSAPP' AKIDANGANYA MTOTO WAKE NI MGONJWA

Jamaa mmoja kutoka Tala, Kangundo nchini Kenya amejikuta katika wakati mgumu kwa kukabiliwa na waumini na wanakijiji baada ya kubainika kwamba aliwahadaa kwamba mtoto wake yupo mahututi hospitali nao wakamchangia pesa za matibabu. 

Duru zinaarifu kwamba jamaa alidai kuwa mwanawe alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kuugua jambo ambalo hamna mshirika hata mmoja alithibitisha.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, jamaa alifungua kikundi cha Whatsapp na watu wakajitolea kumchangia na baada ya watu kutoa pesa alijiondoa bila kusema shukrani huku waliomtolea pesa wakibaki na maswali chungu nzima.

 Semasema zinaarifu kuwa baadhi ya waumini walipompigia simu kujua hali ya mwanawe walishangaa kumpata mteja. 

Watu walipokuwa wakimsaka mzee huyo, mwanawe aliyedaiwa kuwa mahututi hospitalini alirejea nyumbani akiwa mzima.

Inasemekana baadaye buda alipatikana kwenye kilabu kimoja mtaani akiwa amelewa na watu wakamplekea nyumbani kumzomea kwa kuwatapeli.

Mzee alipofika nyumbani inaarifiwa kwamba nusra apatwe na mshtuko wa moyo alipompata mwanawe nyumbani huku baadhi ya waumini wa kanisa lake wakishangaa kwa kumuona akiwa amechapa mtindi kweli kweli.

 “Ziko wapi pesa ulizochangiwa ukidai nilikuwa mahututi hospitali? Mimi niko mzima na sijawahi kuugua tangu nilipoenda mjini,” kijana wa mzee alisema.

Baadhi ya washiriki walimfokea mzee lakini msamaha wake uliambulia patupu.

 “Turudishe pesa zetu mara moja. Wewe ni mtu bure kabisa. Ulikuwa unataka pesa za kwenda kununua pombe! Wewe nitapeli kabisa,” dada mmoja aliwaka.

“Msinipandishe presha bure . Mimi sikulazimisha mtu anitumie pesa na hamfai kunisumbua. Nataka kwenda kupumzika. Fanyeni mtakalo lakini mjue chochote kibaya kikinitendekea ni nyinyi wa kulaumiwa,” mzee alisema.

Chanzo - Tuko news


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com