POLISI ARUSHA WAMDAKA MGANGA WA KIENYEJI KUSHAWISHI MTOTO APIGWE NA KUWEKEWA MAJANI MDOMONI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP- Justine Masejo

Na Abel Paul - Jeshi la Polisi Arusha.

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mganga wa kienyeji (jina limehifadhiwa) mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi mtuhumiwa wa tukio la ukatili dhidi ya mtoto lililotokea tarehe 06 Julai mwaka huu eneo la Burka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP- Justine Masejo akiongea na waandishi wa habari leo Julai 8 mwaka huu jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya mtoto wa kiume mwenye miaka (4) ambaye alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na kutekelezwa katika eneo la Burka tarehe 08.07.2021 muda wa 07:00 mchana huko maeneo ya Sombetini jijini Arusha.

Kamanda Masejo amewaambia waandishi wa habari kuwa katika mahojiano ya kina na mganga huyo wa kienyeji mkazi wa Sombetini ambaye amekiri kumshawishi mtuhumiwa huyo aliyemfanyia ukatili mtoto wa miaka minne (04) ambapo alimshawishi kwamba ukifanya kitendo hicho kitamsaidia katika kesi zake pamoja na utajiri katika biashara.

Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na Upelelezi pindi utakapokamilika Jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za kisheria.

Katika tukio jingine Kamanda Masejo amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia  linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika wilaya ya Monduli kwa tuhuma ya mauaji ya Laisi Lemomo (26) Mfugaji mkazi wa kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

Amesema tukio limetokea tarehe 12.07.2021 muda wa 10:00 jioni  katika kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha.

"Katika kubaini undani wa tukio hilo timu ya makachero imefika eneo la tukio na inaendelea uchunguzi wa tukio hilo na pindi Upelelezi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa ", amesema.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuwashawishi watu kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya kina mama na watoto,kwamba wakifanya hivyo watafanikiwa katika mambo yao mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم