Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akiwaelezea kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwa wananchi waliotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwa ni pamoja na kuonesha Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Wananchi mbalimbali wamejitokeza kutembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na STAMICO ikiwa ni pamoja na kuangalia Mkaa Mbadala unaotokana na Makaa ya Mawe.
Akizungumza leo Julai 26,2021 kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga, Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo amesema wanajivunia mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes unaozalishwa kwa kutumia wataalamu wa shirika la Madini la Taifa.
"Tumeshiriki maonesho haya kwa ajili ya kuonesha bidhaa za STAMICO, tumekuja na mkaa mbadala wa kupikia unaotokana na makaa ya mawe unaitwa Rafiki Briquettes. Mkaa huu ni Rafiki kwa matumizi yake. Lakini mkaa huu ni Rafiki kwa mazingira ukifananisha na nishati ya kupikia inayotokana na miti",amesema Mahungo.
"Cha kujivunia mkaa huu mbadaa unazalishwa kwa kutumia wataalamu wa shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Tunatarajia kuanza rasmi uzalishaji wa mkaa huu mwishoni mwa mwaka huu 2021, tayari mitambo imeagizwa kutoka China",ameeleza.
Amesema pindi uzalishaji rasmi wa mkaa huo utakapoanza na mkaa mbadala kuuzwa nchi nzima utasaidia nchi kuachana na uharibifu wa mazingira kwa utakaji miti ili kupata nishati ya kupikia.
"Pia katika maonesho haya tumekuja kutangaza kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery. Hiki ni kiwanda kikubwa katika Afrika Mashariki na Kati chenye uwezo wa kusafisha dhahabu 480 kg kwa siku kwa kiwango cha kimataifa 99.99%",amesema Mahungo.
Ameongeza kuwa mbali na kusafisha dhahabu pia kiwanda hicho kinanunua dhahabu akisema hiyo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa dhahabu kupeleka dhahabu kiwandani ili kusafisha na kuiuza kwa bei nzuri kwa sababu inakuwa imeongezwa thamani.
Amesema kiwanda hicho kimetoa ajira kwa Watanzania, kinalipa Kodi na tozo mbali za serikali.
Aidha Mahungo amesema kupiti maonesho hayo pia wanatoa elimu kwa wachimbaji wadogo juu ya njia bora na salama za uchimbaji ambapo STAMICO inaendelea kufanya kazi kwa karibu na wachimbaji wadogo ili kuhakikisha nao wanakua na kufikia wa kati na wakubwa
Amebainisha kuwa kwa sasa shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lina vituo vya mfano vyenye mitambo ya kisasa ya kuchenjua dhahabu Lwamgasa, Katente na Itumbi.
Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akiwaelezea kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwa wananchi waliotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na Makaa ya Mawe (kulia) kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwila - Kabulo mkoani Mbeya.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akiwaelezea kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwa wananchi waliotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akionesha Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwa wananchi waliotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akielezea kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akionesha Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akielezea kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akionesha mfano wa Makaa ya mawe yanayotumika kutengeneza Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kushoto) akionesha mfano wa Makaa ya mawe yanayotumika kutengeneza Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Mwananchi akiangalia Sampuni ya miamba yenye madini katika banda la STAMICO na STAMIGOLD Biharamulo Mine (SBM) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Mjiolojia kutoka STAMIGOLD Biharamulo Mine (SBM), Funga Salum Magongo akiwaelezea wananchi kuhusu Sampuni ya miamba yenye madini katika banda la STAMICO na STAMIGOLD Biharamulo Mine (SBM) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin