Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF. MANYA AJIONEA MAAJABU YA CHUO CHA VETA KWENYE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA


Kushoto ni Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Veta Shinyanga, Robert Onesmo akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) kuhusu madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea banda hilo la Chuo cha Veta wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021.

Akiwa katika banda la Chuo cha VETA Shinyanga, Prof. Manya amejionea fani mbalimbali zinazotolewa katika chuo ikiwemo Fani ya Uchongaji na Ung'arishaji wa Madini ya Vito, Fani ya Umeme wa majumbani, Fani ya Saluni na Mapambo na Fani ya Ufundi wa Mitambo na magari makubwa ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya chuo hicho kupata ujuzi mbalimbali.

Akielezea kuhusu fani hizo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele amesema chuo chao kinatoa mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini vito pia mafunzo ya mitambo mizito katika uchimbaji wa madini akibainisha kuwa VETA Shinyanga pekee ndiyo inatoa mafunzo ya aina hizo.

"Kwenye banda letu tunaonyesha mafunzo yanayotolewa na VETA Shinyanga katika fani za uchakataji madini (Ukataji na Ung'arishaji madini vito), Mitambo mizito inayotumika katika uchimbaji madini (uendeshaji mitambo na ufundi mitambo), fani ya umeme na fani ya Ulembeshaji (Salon) na mapambo pia tunatoa huduma za Saluni na ukaguzi wa magari kwenye banda letu",alieleza Mabelele.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Hapi aliitaka VETA ianzishe fani za madini kwenye mikoa mingine pia na kuipongeza VETA Shinyanga kwa kuanza kutoa mafunzo katika sekta ya madini.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) akiangalia madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Hapi
Madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kulia) kuhusu Mashine zinazotumika kukata madini yenye uwezo wa kupitisha mwanga na yasiyo na uwezo wa kupitisha mwanga.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kuhusu Fani ya Ufundi wa Mitambo na magari makubwa
Mwalimu wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Divoti Emmanuel akionesha vifaa vinavyotumika katika ufundi wa mitambo mikubwa na magari makubwa kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga,Veronica Mussa akielezea kuhusu Mfumo wa umeme majumbani kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Rose Silivery akielezea kuhusu Mashine zinazotumika kukata madini yenye uwezo wa kupitisha mwanga na yasiyo na uwezo wa kupitisha mwanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Amida Athumani akionesha madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Husna Rashid akionesha vifaa vinavyotumika katika urembo na upambaji kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Husna Rashid akionesha vifaa vinavyotumika katika urembo na upambaji kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga..Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com