Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY : AJIRA MPYA ZIMEPUNGUZA UHABA WA WALIMU WA SAYANSI


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema kwa Sasa hakuna Shule ya Sekondari ambayo haina Mwalimu wa Sayansi.

Waziri Ummy amesema katika ajira 6,749 zilizotewa Mwezi Juni 2021, Walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 na Walimu wa Hisabati Ni 599 ambao wamesambazwa katika shule ambazo hazikuwa na Walimu hao hapo awali.

“Ni imani yangu sasa hakuna shule yoyote ya Sekondari nchini ambayo haina mwalimu wa sayansi hata mmoja,”amesema.

Hata hivyo, ameiaagiza Mikoa kumleta taarifa iwapo kuna Shule ya Sekondari katika Halmashauri ambayo haina Mwalimu wa masomo ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati hata mmoja ili ufanyike msawazo wa walimu wa Sayansi.

Aidha, amesema katika mwaka huu wa fedha 2021/22 serikali inatarajia kuajiri walimu 10,000 na kipaumbele kitakuwa walimu wa Sayansi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com