Masten Wanjala, Mtuhumiwa wa mauaji ya watoto nchini Kenya
Polisi nchini Kenya wanamshikilia Masten Wanjala (20) anayedaiwa kuua watoto kwa nyakati tofauti aliokuwa akiwakuta wakicheza na kuwahadaa kisha kuwaua kwa kuwanyonga ama kuwafyonza damu na kisha miili yao kuitupa na kwamba alianza kutekekeleza unyama huo akiwa na umri wa miaka 16.
Taarifa hiyo imechapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, na kueleza kuwa kijana huyo amewaua watoto takribani 10 kufuatia mwendelezo wa matukio ya utekaji nyara na mauaji ya watoto nchini humo.
Mara baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo aliwaelekeza maafisa upelelezi maeneo baadhi alikoitupa miili ya watoto aliowaua, ambapo amekiri kwamba amekuwa akitumia kemikali inayofanana na unga kwa wathiriwa kwa kuwalazimisha wainywe ama kuwapulizia usoni kabla ya kuwaua kwa kuwanyonga au kuwafyonza damu kupitia mishipa.
Taarifa zimeongeza kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akiwaua watoto wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 13, huku akihusishwa pia na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kufanyika siku za nyuma