• Kupitia Huduma za “Equity ni Moja” Wateja Benki ya Equity Tanzania sasa wanaweza kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani ya Kusini kama wapo nyumbani.
• Kupitia huduma mpya ya SADCC- SIRESS wateja wa Benki ya Equity wanaweza kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango.
Dar es Salaam, Jumanne tarehe 27 Julai 2021. Benki ya Equity Tanzania leo imeingiza sokoni la huduma mbili mpya za utumaji fedha kimataifa zinazolenga kuingusha Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Huduma hizo ni “Equity ni Moja” ” ambayo inawawezesha Wateja Benki ya Equity Tanzania kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda. Pia Huduma ya SADCC-SIRESS INAYOWAWEZESHA wateja wa Benki ya kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango.
Kulingana na MD, huduma nyingine ni suluhisho la utumaji na upokeaji fedha ndani ya eneo la SADC ijulikanayo kama (SIRESS). "Huu ni mfumo wa kidigitali wa ufanyaji miamala ya kibenki kwa nchi wanachama wa SADC yaani Angola, Botswana, Comoro , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eswatini, Lesotho, Madagaska, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia, na Zimbabwe. Kupitia huduma hizi, wateja wa Benki ya Equity wataweza kufanya miamala ya kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao wetu kwa uharaka na gharama nafuu ya Dola 10 tu kwa muamala bila kujali kiasi kilichotumwa" anasema MD.
Wafanyakazi wa Equity Bank wakipozi kwa picha |
Social Plugin