Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB YAKABIDHI MABATI YA MIL 13.7 KWA SHULE YA SEKONDARI MAGANZO, SONGWA NA ZAHANATI YA ITONGOITALE KISHAPU


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya NMB imekabidhi Mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 13.7 ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari Maganzo na Songwa na ujenzi wa Zanahati ya Itongoitale wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Msaada huo umekabidhiwa leo Jumatano Julai 28,2021 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse kwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Maganzo.

Akikabidhi mabati hayo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse amesema wamekabidhi mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= akifafanua kuwa shule ya Sekondari Songwa imepata mabati 140 yenye thamani ya shilingi 4,560,000/=, shule ya Sekondari Maganzo mabati 158 yenye thamani ya shilingi 5,073,000/= na zanahati ya Itongoitale mabati 180 yenye thamani ya shilingi 5,700,000/=.

Amesema wametoa mabati hayo ikiwa ni moja ya ushiriki wa Benki ya NMB katika maendeleo ya jamii kama Benki inayoongoza nchini Tanzania katika kuhakikisha jamii inafaidika kutokana na faida wanayopata.

“Sisi NMB tulipopata maombi yenu ya uhitaji wa mabati tulifarijika na kuamua kuja mara moja kushirikiana na ninyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu na afya kwa jamii yetu ikizingatiwa kuwa Benki ya NMB imejikita zaidi kwenye maeneo ya elimu na afya”,ameongeza Magesse.

Amebainisha kuwa changamoto za sekta ya elimu na afya Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele kwani elimu ndiyo ufunguo mkuu wa maendeleo kwa taifa lolote na ili wananchi waweze kuleta maendeleo ni lazima wawe na afya lakini pia kupitia jamii ndiko wateja wao wanapotoka hivyo umekuwa utamaduni wao kurudisha kwa jamii faida wanayopata.

“Tunatambua juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu za kusimamia sekta ya elimu na afya kwa nguvu zote. Pamoja na mambo makubwa yanayofanywa na serikali, sisi kama wadau tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii zetu kwani kupitia jamii hii hii ndiyo imeifanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote nchini”,amesema Magesse.

“Kwa miaka kadhaa sisi NMB tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii. Mwaka huu tumetenga shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia kuboresha sekta ya elimu na afya nchini”,ameongeza Magesse.

Aidha amesema Benki ya NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga elimu na afya bora kwa jamii ya Kitanzania.

“NMB imezifikia wilaya zote nchini kwa asilimia 100 na tunaendelea kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mitandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi zaidi. Tunahamasisha wakulima, wafugaji,wajasiriamali na wafanyabiashara kutumia huduma za benki ya NMB”,amesema.

“Benki ya NMB ndiyo Benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi 226, ATM zaidi ya 8000 nchi nzima, NMB Wakala zaidi ya 8,000 pamoja na wateja zaidi ya Milioni 3 idadi ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha na Benki zingine nchini”,ameeleza Magesse.

Akipokea mabati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude ameipongeza Benki ya NMB kwa mambo mema inayoendelea kuyafanya ambayo ni kipaumbele cha taifa na kuwa mstari wa mbele kutoa misaada kwa jamii kila mara.

“Tunawashukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia sekta ya elimu na afya. Hii siyo mara ya kwanza kusaidia hapa wilaya ya Kishapu, hata haya madawati wanayotumia wanafunzi katika shule hii ya Maganzo yalitolewa na Benki ya NMB”,amesema Mkude.

Ametumia fursa hiyo kuiomba Benki ya NMB kutochoka kusaidia jamii huku akiwaomba wadau wengine kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii akisema bado baadhi ya shule za Kishapu zina upungufu wa miundo mbinu ikiwemo madawati na madarasa.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kutunza madarasa na madawati ili yadumu kwa muda mrefu.

Naye Diwani wa kata ya Maganzo, Mbalu Kidiga amesema Benki ya NMB imekuwa mdau mkubwa na imesaidia pakubwa katika kata yake ikiwa ni pamoja kusaidia ujenzi wa madarasa na madawati.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza leo Julai 28,2021 wakati akipokea mabati yaliyotolewa na Benki ya NMB yenye thamani ya shilingi Milioni 13.7 ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari Maganzo na Songwa na ujenzi wa Zanahati ya Itongoitale wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akiipongeza Benki ya NMB kwa kusaidia mabati 478 yenye thamani ya shilingi Milioni 13.7 ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari Maganzo na Songwa na ujenzi wa Zanahati ya Itongoitale wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akielezea kuhusu msaada wa mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa ambayo imepata mabati 140 yenye thamani ya shilingi 4,560,000/=, shule ya Sekondari Maganzo mabati 158 yenye thamani ya shilingi 5,073,000/= na zanahati ya Itongoitale mabati 180 yenye thamani ya shilingi 5,700,000/=.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi mabati kwa ajili ya Shule za Sekondari Maganzo na Songwa pamoja na Zahanati ya Itongoitale. Amesema Benki ya NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga elimu na afya bora kwa jamii ya Kitanzania.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (wa nne kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale.

Zoezi la makabidhiano ya mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale likiendelea.

Zoezi la makabidhiano ya mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale likiendelea.

Zoezi la makabidhiano ya mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale likiendelea.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maganzo wakipiga makofi wakati wa zoezi la makabidhiano ya mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale.

Meneja Mahusiano Serikali na Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Bi. Vivian Nkhangaa (kulia) akifuatiwa na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Maganzo, Daniel Rauya na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya mabati 478 yenye thamani ya shilingi Milioni 13.7 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale likiendelea.

Diwani wa Kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu, Mhe. Mbalu Kidiga akiishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya mabati na madawati.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Maganzo, Shija Mbuzi Mbili akizungumza wakati Benki ya NMB ikikabidhi mabati 478 yenye thamani ya shilingi 13,767,300/= kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Songwa , shule ya Sekondari Maganzo na zanahati ya Itongoitale.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com