Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BROTHERHOOD SURVEY SERVICES YATANGAZA MCHONGO WA VIWANJA IBADAKULI

Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani mahali ulipo mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited ya Mjini Shinyanga imeshiriki Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha huduma wanazotoa pamoja na kuwatangazia wananchi kuhusu mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 31,2021 Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi amesema Kampuni yao inajihusisha na Uendelezaji wa ardhi, ushauri kuhusu masuala ya ardhi, usimamizi wa mali yakiwemo majengo, magari na viwanja, ukusanyaji wa ushuru na mikopo, udalali, uchoraji wa ramani za majengo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.

Amesema Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Ltd imeshiriki kwenye Maonesho hayo kwa ajili ya kuonesha huduma wanazozitoa.

“Kwenye maonesho haya pia tumekuja kuwatangazia wananchi kuhusu mradi wetu wa uuzaji Viwanja unaojulikana kwa jina la Diamond City Project unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga",amesema.

“Mradi huu wa viwanja upo Kilomita 8 kutoka Mjini Shinyanga na mita 500 kutoka barabara kuu ya Shinyanga - Mwanza. Katika mradi huu tunauza viwanja kwa bei nafuu kuanzia shilingi 540,000/= na unaweza kulipa kidogo kidogo hadi miezi sita. Viwanja vimepimwa na pia Kampuni yetu itafuatilia upatikanaji wa Hati Miliki ya Kiwanja chako kama utahitaji”,ameongeza Victoria.

Eneo la mradi huo wa uuzaji viwanja lipo jirani na mahali patakapojengwa Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga, Ibadakuli eneo ambalo ni zuri kwa uwekezaji wa biashara na viwanda vidogo vidogo lakini rafiki kwa makazi na tayari kuna huduma ya umeme ,maji na zahanati ya Ibadakuli.

Ofisi za Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited zipo Mjini Shinyanga jengo la NSSF Mafao ghorofa ya Pili Wasiliana nao zaidi kwa simu namba 0746633364 ,0768992606, 0754 763263,0757462260 au Email
 info@brotherhoodsurveyservices.com
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani mahali ulipo mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Julai 31,2021 kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akionesha ramani  ya nyumba kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akielezea kuhusu huduma zinazotolewa na Kampuni yao kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Victoria Mahindi akiwakaribisha wananchi kuchangamkia fursa ya viwanja wanavyouza kupitia mradi wao wa uuzaji wa Viwanja ‘Diamond City Project’ unaopatikana katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Ofisi za Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited zipo Mjini Shinyanga jengo la NSSF Mafao ghorofa ya Pili Wasiliana nao zaidi kwa simu namba 0746633364 ,07689926060754 763263,0757462260 au Email
 info@brotherhoodsurveyservices.com


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com