Msimamizi wa Uchaguzi wa viongozi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga Bi. Shani Kibwasari ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu TALGWU
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga, Dkt. Martine Dotto Mazigwa Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa
Shinyanga wamefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali ambapo wamemchagua Dkt. Martine Dotto Mazigwa kuwa
Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha
miaka mitano.
Uchaguzi huo
umefanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 wakati Mkutano Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga
uliofanyika katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi Bi. Shani Kibwasari ambaye ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu amesema wagombea nafasi
ya Mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Shinyanga walikuwa Dkt. Martine Dotto Mazigwa, Nyalali Thomas Ndaki, Robert Kaunda Sospeter ambapo Dkt. Martine Mazigwa ameibuka mshindi wa kiti hicho.
Nyalali Ndaki amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Nunya Chege Mjumbe wa Kamati ya Utendaji taifa pamoja na viongozi wengine wa nafasi mbalimbali.
Awali akifungua
Mkutano Mkuu wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga, Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston
Mizengo amewataka wanachama wa TALGWU kuhakikisha wanakiunga mkono chama hicho
ili kiweze kuendelea kuwahudumia wanachama wake.
Mizengo amesema
hakuna haki bila wajibu hivyo wanachama na watumishi wa TALGWU wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao ili hata pale wanapodai haki basi hiyo
haki iwe inastahili.
Mizengo
ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi anazotoa kwa wafanyakazi
akibainisha kuwa Rais Samia anatekeleza kile anachosema.
“Tunatumia
nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi aliyoitoa kwenye Siku ya Mei Mosi mwaka
2021 jijini Mwanza, aliahidi mambo mengi kwa watumishi ikiwemo kuwapandisha
madaraja,nyie wafanyakazi ni mashahidi si mmeona?, ee kwa hiyo tuna Rais ambaye
anasema halafu anatekeleza”,amesema Mizengo.
“Mimi ninavyojua
nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi, tujitahidi kumuunga mkono Mheshimiwa
Rais Samia na tunamuunga mkono Rais
Samia kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa,kufanya kazi kwa nidhamu,kufanya
kazi kwa kuhakikisha kwamba taifa letu linasonga mbele”,ameongeza Mizengo.
“Kingine
alichotufanyia Rais Samia si mnakumbuka wale waliokopa mikopo ya elimu ya
juu,ile tozo ya asilimia 6 aliifuta, lakini pia kodi kwenye mishahara yetu Mhe.
Rais Samia alipunguza asilimia moja kutoka asilimia 9 hadi 8 ambapo zamani kodi
ilikuwa inafikia hadi asilimia 16”,amesema.
Hata hivyo amesema
mafanikio yote yaliyopatikana siyo kwamba yamepatikana from No where ni kwa
jitihada za viongozi wenu mliowachagua kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali
wakiwemo wa TUCTA katika kuisukuma serikali ili kuhakikisha inatekeleza yale
iliyoyaahidi kwa wafanyakazi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. Mkutano huo umekwenda sanjari na uchaguzi wa viongozi wa TALGWU. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. Mkutano huo umekwenda sanjari na uchaguzi wa viongozi wa TALGWU.
Awali Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga, Maximilian Lugemba akizungumza kwenye Mkutano huo uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga.
Katibu wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga, Ally Ernest akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga.
Kidana Milando akisoma taarifa ya Kazi na Fedha kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga, Maximilian Lugemba na waliokuwa viongozi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga wakijiuzulu kupisha uchaguzi wa viongozi wapya.
Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga.
Msimamizi wa Uchaguzi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga Bi. Shani Kibwasari ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu akitangaza utaratibu wa uchaguzi wa viongozi leo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. Afisa Kazi wa TALGWU mkoa wa Mwanza, Bi. Sabina akitoa mwongozo wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) .
Aliyekuwa Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti wa TALGWU mkoa wa Shinyanga , Bi. Regina Shija Maneno akitangaza kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kuomba kura.
Dkt. Martine Dotto Mazigwa akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga.
Nyalali Thomas Ndaki akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga
Robert Kaunda akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga
Sospeter Nyamuhanga akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga wakipiga kura kuchagua viongozi wao

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
k Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiimba wimbo wa Mshikamano bila kugusana mikono.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiimba wimbo wa Mshikamano bila kugusana mikono.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin