Mratibu wa CHF mkoa wa Tanga Imani Rwatamabanga akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
Mganga Mkuu wawilaya ya Mkinga (DMO) akizungumza wakati wa uzinduzi |
Mratibu
wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson
akieleza umuhimu wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) katika uzinduzi huo |
KATIBU Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kushoto akifuatilia kwa umakini matukio wakati wa uzinduzi huo |
NA OSCAR ASSENGA, MKINGA
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga,Kanali Maulidi Surumbu amewahamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa ili kuweza kupata matibabu wanapougua na hivyo kuwaondolewa changamoto ambazo wanaweza kukutana nazo.
Kanali Surumbu aliyasema hayo wakati akizindua kampeni ya Uhamasishaji wananchi wa Mkinga kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa iliyofanyika kata ya Maramba wilayani Mkinga.
Alisema mpango huo ni mzuri kwa sababu una wahakikishia huduma ya matibabu pindi wanapougua na hivyo kupunguza kiasi kikubwa cha changamoto za kupata huduma za matibabu na kusaidia kuboresha huduma za afya kwenye vituo husika.
“Mwanachama anapojiunga na CHF kuna asilimia 10 ambazo hurudishwa kwenye vituo vya afya hivyo nitumie nafasi hii kuwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mkinga kuhakikisha mnachangamkia mpango huu “Alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema wilaya hiyo ilianza kusajili wanachama kwa kutumia mfumo wa kieletroniki Januari mwaka jana na kaya wanafika watu wasiozidi sita wanapata matibabu kwenye wilaya ya Mkinga na Mkoa wa Tanga kwa miezi 12.
“Mpaka kufikia leo 26,Julai Mkinga imesaijili kaya 661 kati ya kaya 6071 zilizotakiwa kusajili kwa mwaka kati ya hizo kata 661 zilizosajiliwa kaya 506 zimechangiwa na wafadhili,kaya 155 wananchi wa mkinga wamejiunga kwa hiari hivyo ni sawa na asilimia 2.7 ya lengo iliyowekewa wilaya hiyo kwa mwaka”Alisema
Alisema hali hiyo inaonyesha wananchi Mkinga bado hawajahamasika vya kutosha kuhusu umuhiumu wa kujiungaa na mfuko wa afya ya jamii hivyo kupitia kampeni hiyo ambayo inaizindua itakwenda kuwa chachu ya kuhamaksisha kuwa juu ya uhumu wa kujiunga mfuko wa afya ua jamii iliyoboresha.
“Kauli mbiu ya kampeni hii inasema CHF iliyoboreshwa kwa afya ya kila mtanzania jiunge leo hivyo ni matarajio yangu kwamba baada ya uzinduzi huo wananchi wote mtajiunga na kujisajili”Alisema
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii Mkoa wa Tanga Imani Rwatamabanga alisema lengo la kitaifa kwa CHF ni kufikia asilimia 30 ya watanzania wote wanaopaswa kujiunga na CHF ifikapo June 2021 sasa leo ni Julai mwisho ni asilimai 30 kwa Taifa.
Alisema kwa mkoa wa Tanga ili kufikia lengo hilo la asilimia 30 ya wakazi wa mkoa huo walipaswa kufikia kaya zipatazo 146,954 hadi June 2021 katika kufikia lengo hilo mkoa unapaswa kuandikisha kaya 14,695 ambao ni sawa na asilimia 3 kwa kila mwezi,Kaya 48,985 ambayo ni sawa na asilimia kwa robo mwaka na kaya 146,954 ambayo ni asilimia 30 kwa mwaka.
Aidha alisema takwimu za leo kwa wilaya hiyo kwa mujibu wa tamisemi ina watu 137,268 sawa na kaya 27,454 kama walikuwa wanataka kwenda vizuri kila mwezi walipaswa kusajili kaya 824 na robo mwaka wawe wamesajili kaya 2,745 ambapo wangekuwa wamesajili kwa mwaka kaya 8,230 ambayo ingewapa asilimia 30.
Alisema hadi asubuhi kaya ambazo zimesajiliwa ni 155 hivyo kwa pamoja viongozi viongozi ,wananchi washirikiane wameane hamasa ili kuweza kuongeza idadi ya kaya ambazo zitakuwa zimesajiliwa.
Hata hivyo kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson alisema mfuko huo unafaida kubwa sana kwa wananchi hivyo wanapaswa kuchangamkia kujiunga nao ili waweze kunufaika na huduma za matibabu katika vituo vya Afya.
Alisema fursa hiyo ni muhimu na nzuri hivyo wajitokeze kujiunga ili kuweza kunufaika na mfuko huo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkinga Amani Kasinya alisema mpango huo ni mzuri na ni matunda ya serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma za Matibabu.
Kasinya aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanachangamkie mfuko huo ambao unafaida kubwa kwao kutokana na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapokuwa wakiugua.