Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ENGLAND YASHINDWA NA ITALIA 3-2 KUPITIA PENALTI


Matumaini ya kumaliza ukame wa miaka 55 bila taji kubwa yalivunjwa jana kwa kushindwa na Italia kupitia mikwaju ya Penalti na kuipa Italia ushindi wa kombe la Euro 2020 uwanjani Wembley

Italy, ambao hawajashindwa katika mechi 33 kabla ya fainali walijirejesh polepole mchezoni na wakasawazisha katika dakika ya 67 baada ya England kutangulia kufung mapema katika kipindi cha kwanza .

Baada ya kipindi kigumu cha muda wa ziada ,mshindi hakupatikana timu hzo zilipotoka sare ya bao moja na ikalazimu mikwaju ya penalti kutumiwa kumpata mshindi .Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafadhaiko ya kocha Gareth Southgate na wachezaji wake walioingia fainali kwa matumaini makubwa .
England ilikosa kufunga mikwaju mitatu ya penalti kati ya mitano waliopewa huku wachezaji Marcus Rashford ,Jadon Sancho na Bukayo Saka wakikosa kufunga


Harry Kane na Harry Maguire waliifungia England ilhali Pickford mikwaju ya Andrea Belotti na Jorginho ilhali Domenico Berardi, Bonucci na Federico Bernardeschi waliifungia Italia.
Kikosi cha Italia

Kushindwa kwa England kwa Euro 2020 na Italia ni "chungu mno" lakini wachezaji walijitolea kwa hali na mali', alisema meneja Gareth Southgate.

The three Lions , walishiriki kwenye fainali yao ya kwanza kwa wanaume kwa miaka 55, na walishindwa kupitia penalti kufuatia ya sare 1-1 baada ya dakika 120.

"Sisi sote tuko pamoja. Wameipa nchi kumbukumbu zisizoweza kuaminika," Southgate alisema kwenye BBC One.

Nahodha Harry Kane alisema kushindwa huko "kutaumiza muda uliosalia wa taaluma zetu ".

Furaha kwa Italia

Kocha a Italia Roberto Mancini naye amesema 'alistahili kushinda kombe hilo' baada ya kikosi chake kuishinda England kupitia penalti.

Mancini alikosa kushinda kombe kubwa kama mchezaji na Azzurri, wakimaliza wa tatu katika Italia 90 na mshindi wa pili kwenye Mashindano ya Uropa ya Vijana chini ya miaka 21 mnamo 1986.

"Nilibahatika sana kucheza katika kikosi hiki mnamo 1990 na timu kali ya chini ya miaka 21 mnamo 1988," alisema.

"Licha ya ukweli kwamba tulikuwa timu bora, hatukushinda na tukapoteza mara mbili kwa mikwaju ya penalti."

Baada ya kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2018, Italia wamefurahia mabadiliko makubwa chini ya Mancini, na hawajafungwa katika michezo 34.

Kocha huyo wa zamani wa Manchester City alisema machozi yake baada ya mchezo huo yalikuwa kwa Italia nzima.

Saka mwenye umri wa miaka 19 aliyejawa machozi, ambaye alionyesha ujasiri kama kwa kusonga mbele, alifarijiwa na wenzake katika timu na meneja Southgate lakini hakukuwa na faraja ya kweli kwao au mashabiki waliotarajia ushindi ambao walijaa ndani ya Wembley.


England haikuweza kumudu kuzuia ushindi wa Italia

Miaka mingi ya kungoja kwa England iliendelea lakini katika dakika 30 za kwanza za fainali kulikuwa na matumaini kwamba wakati ambao nchi imesubiri zaidi ya siku 20,000 ulikuwa umefika.

Safari za timu hizi kuingia fainali

Italia ilianza safari ya kufika fainali ya mwaka huu ya Euro kwa kushinda mechi zake zote za kundi A kwa kuichapa Uturuki 3-0, ikailaza Switzerland 3-0 kabla ya kuilaza Wales 1-0. Hatua ya 16 bora ikaichapa Austria 2-1, ikakutana robo fainali na Ubelgiji ikawalaza 2-1 kabla ya kuiondosha kwa matuta 4-2 Hispania baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1.
Kikosi cha England

England iliyowaondoa Denmark katika nusu fainali kwa kuichabanga 2-1, ilianza safari yake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Croatia, ikaenda sare tasa ya 0-0 na ndugu zao wa Scotland kabla ya kumaliza michezo yake ya kundi D kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Czech Republic. 16 bora ilikutana na Ujerumani ikapata ushindi wa kihistoria wa mabao 2-0 kabla ya kuiondosha Ukraine kwenye robo fainali kwa kapu la mabao 4-0

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com