Msanii wa Afro Beat,Rhumba,Hip
hop na R & B Sawyer Misibumba maarufu kwa jina la Homahoma kutoka nchini Congo ambaye makazi yake ni huko nchini Ubelgiji ni mmoja wa msanii wenye
talanta ya kipekee sana kuanzia uandishi wake katika muziki.
Homahoma aliamua kufanya mziki
rasmi tangu mwaka 2019 ambapo aliachia kazi yake ya “Baby Dose” iliyofanikiwa
kwa kiasi flani na baadaye kuja kuachia kazi yake nyingine ambayo ilipewa jina
la “Pakadjuma” ambayo ilikuwa na miondoko ya Afro Beat huku akivutiwa na
wasanii kama Wizkid pamoja na Burnaboy kutoka Nigeria.
Talanta ya Homahoma ilianza
kuonekana baada ya msanii huyu kuwa mpenzi sana wa muziki wa Papa Wemba,Koffi Olomide kutoka Congo lakini pia katika kizazi chake alipendezwa zaidi na
muziki wa Kanyewest,Stromae na Amigos.
Homahoma ameachia kazi yake
mpya kutoka kwenye Ep yake iitwayo “Hopium” na wimbo huo unaitwa Uio. karibu
utazame na unaweza kufuatilia kazi zake kupitia youtube channel yake pamoja na
mitandao ya kijamii kwa jina la @officialhomahoma.
Social Plugin