Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HOSPITALI YA MASWA YAPINGA HABARI ZA UHABA WA DAWA


Samirah Yusuph.
Maswa.
Kufuatia tetesi zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kukosekana kwa dawa hata "Panadol"  katika hospitali ya wilaya ya Maswa, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Fredrick Sagamiko amesema taarifa hiyo sio sahihi.

Sagamiko amesema kuwa hali ya upatikanaji wa madawa katika hospital ya wilaya hiyo ni asilimia 98 na upatikanaji wa madawa muhimu ni 100 na kuwa halmashauri hiyo inaduka la madawa bora miongoni mwa maduka yote ya madawa nchini.

"Taarifa hiyo haina ukweli, kuna dawa za kutosha na duka la dawa linalo milikiwa na hospital ya wilaya ya Maswa ndilo duka linalouza dawa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za Mkoa wa Simiyu pia tuna mfumo wa "hospital protocol" unaowezesha ofisi ya mkoa kupata taarifa za utoaji wa dawa kwa kila wiki kwa hospitali zote"

Ameongeza kuwa hapo mfumo wa utoaji taarifa za dawa katika ofisi ya mkuu wa wilaya imesaidia kuondoa kwa kiasi kikubwa upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo dawa stahiki zinawafikia wahitaji bila kuwa na shaka.

Aidha kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali hiyo James Bwire alisema kuwa mahitaji ya dawa katika hospitali hiyo yanajitosheleza na kuwa hospitali hiyo inamaduka matatu ya dawa ambalo ni duka la wateja wa bima, duka linalo hudumia zahanati, vituo vya afya na hospitali nyingine pamoja na duka la hospital.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Binza Aroni Joseph Mboje alisema kuwa shida na madawa ilikuwepo kipindi cha nyuma lakini kwa sasa haipo tena mambo yanayo jitokeza katika mikutano sio uhalisia kwa sasa dawa zipo za kutosha.

"Vitu wanavyovisema wananchi hawana uhakika navyo baada ya taarifa hiyo nilifika hospitali kuja kujionea lakini kuna dawa nyingine wanaandikiwa wakachukue maduka ya nje hivyo wanasema hospitali haina dawa lakini dawa zipo za kutosha".

 Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com