JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) LALAANI MSEMAJI WA SIMBA HAJI MANARA KUMDHALILISHA MWANDISHI WA HABARI

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitika na kulaani kitendo cha msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara kumdhalilisha mwandishi wa Habari wa Redio Clouds FM, Prisca Kishamba.


Taarifa iliyotolewa na jukwaa hilo leo Ijumaa Julai 2, 2021  na mwenyekiti wake, Deodatus Balile inaeleza kuwa udhalilishaji huo ulioambatana na maneno ya kashfa ulifanywa  kwenye mkutano wa Simba na waandishi wa habari uliofanyika Juni 30, 2021 mkoani Dar es Salaam.

TEF imemtaka Manara kuacha mara moja tabia ya kutumia mikutano ya klabu ya Simba na hata mitandao ya kijamii kuwadhalilisha wanahabari.

Limesema ikiwa kuna suala lolote ambalo mwandishi wa habari amelitenda kinyume cha maadili na miongozo ya taaluma, wahusika wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa taasisi za kihabari au kwa mwajiri wa mwandishi husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kupitia taarifa hiyo,  TEF imeuomba uongozi wa timu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumuonya Manara kuacha tabia hizo mara moja kwani  hazina afya na haziongezi thamani yoyote kwa Simba wala taaluma  ya habari.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post