Mwanaume anayetuhumiwa kujaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali, Assimi Goïta, wiki iliyopita msikitini amekufa hospitalini akiwa chini ya ulinzi, serikali inasema.
Mshambuliaji huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio lake, ambalo lilifanyika wakati Bwana Goïta akihudhuria sala katika msikiti.
Taarifa ya serikali ilisema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini, ambako alikufa.Sababu ya kifo chake inachunguzwa .Bwana Goïta ameongoza mapinduzi mawili nchini Mali katika mwaka uliopita.
Social Plugin