Makamba ametoa kauli yake hiyo hii leo Julai 26, 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter, mara baada ya uwepo wa video clip zinazosambaa mitandaoni zikimuonesha mbunge huyo wa Kawe akidai kuwa Tanzania ilikuwa imeshashinda Corona na kwamba chanjo ya Corona ni mpango wa mataifa ya nje kuwaangamiza Watanzania.
"Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki, ni hatari kupotosha watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo, mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba serikali imeileta kuwadhuru watu si sahihi," ameandika Makamba.
Juzi Jumamosi ya Julai 24, 2021, Tanzania ilipokea dozi zaidi ya milioni 1 za chanjo ya Corona kutoka Marekani kupitia mpango wa usambazaji chanjo ya Corona wa COVAX.
Social Plugin