Mbunge
Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) Mhe. Neema
Lugangira akiwasilisha mchango wa Taulo za Kike kwa wanafunzi 42 mwaka
mzima (dozen 42, packet 504), katika Ofisi za EATV, Mikocheni ikiwa ni
kuunga mkono kampeni ya Namthamini
Mbunge
Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) Mhe. Neema
Lugangira amewasilisha mchango wa Taulo za Kike kwa wanafunzi 42 mwaka
mzima (dozen 42, packet 504), katika Ofisi za EATV, Mikocheni ikiwa ni
kuunga mkono kampeni ya Namthamini.
Akizungumza
baada ya kukabidhi mchango huo amesema kuwa kampeni ya Namthamini
isiishie tu kwa wanafunzi mashuleni lakini pia ifike katika Magereza ili
kusaidia pia wafungwa na mahabusu wakike ambao taulo hizo za kike pia
ni changamoto kwao.
“Nimeguswa
na kampeni ya Namthamini na nimekuwa nikifanya hivyo kupitia Taasisi ya
Agri Thamani ambayo mimi ni Mkurugenzi kwa lengo la kuhakikisha
tunasaidia Watoto wa Kike kubaki Shule hasa madarasa yale ya mitihani
(Kidato cha 2 na cha 4) ili Watoto hawa wasipoteze ndoto zao. Kwa mwaka
huu 2021 kupitia Agri Thamani tulitoa Taulo za Kike za Mwaka Mzima kwa
Wanafunzi wa Kike 1,800 wa Sekondari 16 za Kata za Bukoba Manispaa,
Kagera kwa Kidato cha 2 na cha 4 na pia tulitoa kwa Wanafunzi wa Kike
3,700 wa Sekondari kutoka Mikoa 19 Tanzania Bara na Zanzibar na
tutafanya tena mwakani 2022”, amesema Mh. Lugangira.
Mheshimiwa
Lugangira amesema pia yeye kama Mbunge amekuwa akitoa Msaada wa Taulo
za Kike kwa Wafungwa na Mahabusu Wanawake ambao nao pia wanauhitaji
mkubwa na mara nyingi wanasahaulia.
Akiwa
kama Mdau wa Masuala ya Local Content, Mh. Lugangira alisisitiza
umuhimu wa kuthamini Viwanda vya Ndani vinavyozalisha Taulo za Kike
zenye Ubora zinatakiwa kupewa nguvu katika uzalishaji wake kwa kuunga
mkono wafanyabiashara wa ndani.
“Nimeleta
taulo hizi ambazo zinatengenezwa na kiwanda cha ndani chenye uzoefu wa
zaidi ya miaka 40 ili kusisitiza Uzalendo kwanza kwa vitendo, tuthamini
vya ndani na suala la hedhi salama kwa wanafunzi wa kike, wafungwa na
mahabusu wa kike imekuwa ni moja ya hoja zangu hata ninapokuwa Bungeni”,
amesema Lugangira.