MFANYABIASHARA TABORA ATIWA MBARONI KWA KUKUTWA AKIUZA VIFAA TIBA NA DAWA AMBAZO NI MALI YA SERIKALI


Na Lucas Raphael,Tabora  -TDMA
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya magharibi imefanikiwa kumkamata mfanyabiashara Zakayo Bagomwa aneyemiliki Duka la Dawa  muhumu ilinaloitwa Maliza na Yesu  akiuuza dawa za kifua kikuu TB ,kadi za kliniki za Kina mama Wajawazito, kutoa huduma za matibabu ndani ya duka , vifaa tiba mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kenya vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4,869,900.

Akizugumza na waandishi wa habari leo Kaimu meneja wa Mamlaka ya hiyo kanda ya magharibi Christopher Migoha alisema kwamba tukio hilo litokea julai 20 mwaka huu mara baada ukaguzi maalumu wa duka la dawa katika Kijiji cha Kanindo, Kata ya Kanindo, Tarafa ya Ulyankulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.

Alisema kwamba katika duka hilo  walikuta  Dawa za Serikali ya Tanzania zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Kifungu cha 312(1) cha Kanuni ya Adhabu Sura 16.

Alisema kuwa walikuta Vitendanishi vya kupima UKIMWI pamoja na Vitendanishi vya kupima Malaria ambavyo ni Mali ya Serikali ya Tanzania vikiwa vimehifadhiwa na kutunzwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Sheria.

Aidha kaimu meneja huyo alisema kwamba kwenye duka hilo kulikuwa na  Dawa zisizosajiliwa kutumika nchini zikiwa zimehifadhiwa na kuuzwa kinyume cha Sheria 

Migoha aliendelea kusema kwamba ndani duka  walikuta dawa mali ya Serikali ya Kenya zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa  .

Alisema kwamba ndani ya duka hilo walikuta dawa zisizoruhusiwa kuuzwa katika maduka ya dawa muhimu na kukuta  dawa zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha kanuni ya 63 ya Makundi ya Dawa ya Mwaka 2015.

Hata hivyo meneja huyo wa kanda ya magharibu alisema kwamba walikuta  dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Kifungu cha 75(1) cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Sura 219.

Alisema kwamba mmiliki hyo hakuweza kuwasilisha risiti za manunuzi wala mauzo ya dawa zote alizokutwa nazo kinyume cha  Kanuni za Uendeshaji wa Biashara ya Dawa za Binadamu.

Migoha aliendelea kusema kwamba kulikutwa Vifaa Tiba ambavyo ni Seti ya  kufanyia tohara vikiwa vimetunzwa kinyume cha Sheria pamoja na dawa za wangojwa wa kifuu kikuu ambazo hazikustahili kuwepo ndani ya duka hilo wala kuunzwa kwenye maduka ya dawa muhimu.

Aidha aliwataka wadau  wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) na  Wafanyabiashara wote wa bidhaa za Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi kufanya biashara zao kwa kuzingatia Sheria ya Dawa na Vifaa tiba Sura 219 pamoja na Sheria zingine    .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post