Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mshirika wa Price Water house Cooper (PwC), Bw.Nelson Msuya wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Steve Michael wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo nchiniwakifuatilia hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Wauza pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga wakipatiwa vyeti mara baada ya kufanya vizuri katika sekta hiyo.Zoezi la utoaji vyeti limefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Sekta ya mifugo sasa inachangia uchumi wa nchi zaidi ya asilimia 7.4% na mwaka huu wa fedha unaoisha, sekta hii inakuwa kwa asilimia 5% lengo likiwa kufikia mara mbili kwenye mchango wa uchumi na kuweza kufikia angalau asilimia 15 ifikapo mwaka 2025.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Amesema uzalishaji wa maziwa nchini umefikia bilioni 3.4 ikiwa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni 75 hii inamaana inaleta wawekezaji wengi kuja kuchakata na kuleta thamani kwasababu wateja wananunua maziwa ambayo yameongezwa thamani .
"Takwimu zinaonesha katika lita bilioni 3.4 maziwa yanayotka kwenye ng'ombe wa kienyeji ni lita bilioni 2.38 kwahiyo lita bilioni 1.2 tu zinaonesha zinatokana na ng'ombe wa maziwa". Amesema Prof. Ole Gabriel.
Aidha amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ambapo inazaidi ya ng'ombe milioni 33.9 na mbuzi wameshafika zaidi ya milioni 22 wakati kondoo wamefika takribani milioni 6, kuku wamefikia milioni 87.7.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema amesema kuwa kupitia mradi huo wana matokeo mazuri wameyaona ambapo kuna ng'ombe 558 tayari wana mimba na wengine tayari wameshapata watoto pia kuna ng'ombe 336 ambao wameogeshwa kitaalamu na vilevile kuna ng'ombe 62 ambao hao wamepata chanjo kuanzia mbili na kuendelea.
"Wauza pembejeo hawa wameweza kuwafikia wafugaji 2776 na kuuza pembejeo nne ambazo ni vidhibiti vimelea, Chanjo, lishe uhimilishaji pia mpaka sasa tuna ng'ombe 17,000 ambao wamepata huduma mbalimbali za lishe katika kuongeza afya bora na pia kuweza kupata maziwa yaliyobora". Amesema Bi.Mrema.
Amesema kuwa mradi huo una malengo matatu ambapo lengo la kwanza ni kuongeza uzalishaji na tija ya maziwa kwa wafugaji wadogowadogo, kuongeza kipato kwa wafugaji wadogowadogo wa maziwa, kuleta uwiano sahihi na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa shughuli katika sekta ya maziwa .
Hata hivyo Bi.Mrema amesema washiriki sita wa mradi huo kutoka sekta binafsi wamepata tuzo na motisha ya dola za kimarekani 27,000 kwa pembejeo 4116 zilizokamilika ili waweze kuendelea kutoa huduma na kuongeza uzalishaji wa maziwa na kukidhi soko la Tanzania.
Social Plugin