Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) leo katika maonesho ya 45 ya Saba Saba. Pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri A. Mahimbali
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri A. Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah watembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority - PURA) kwa lengo la kujionea kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi hiyo katika maonesho ya 45 ya Saba Saba. Viongozi hao walitembelea Banda la PURA siku ya Jumapili tarehe 04 Julai, 2021.
Katika maonesho hayo ya Saba Saba, PURA inaeleza wananchi majukumu mbalimbali inayoyatekeleza yakiwemo kuishauri Serikali juu ya masuala ya mkondo wa juu wa petroli; kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli; na kusimamia shughuli zote za miradi ya kusindika gesi asilia kuwa kimiminika.
Social Plugin