Umewahi kufikiria kuwa na mume mwenza katika ndoa? Swali hili ni kwa wanaume, lakini kwa wanawake umewahi kufikiria kuolewana wanaume wawili? Au Unakumbuka tukio la mkazi mmoja wa Makueni huko Kenya, Rael Mukeku, aliyeamua kuolewa na wanaume wawili lilivyosambaa kwenye vyombo vya habari? Ama tukio la Maurine Atieno kutoka eneo la Migori nchini humo alivyotiwa nguvuni baada ya kukiri kuolewa na wanaume wawili?
Ni kawaida hasa kwa jamii ambazo imani ya kiislamu imetawala, kuona mwanaume akiwa na mke zaidi ya mmoja, lakini si jambo la kawaida hasa kwa jamii nyingi kuona wanaume wawili wakimuoa na kuishi na mwanamke mmoja.
Yapo mataifa duniani ambayo ndoa ya mwanamke mmoja kuolewa na wanaume wawili ni kitu cha kawaida kabisa kupitia mila za makabila yao na kuwekewa utaratibu unaotambulika. Ifuatayo ni orodha ya mataifa matano ambayo mwanamke kuolewa na wanaume wawili au zaidi ni jambo linalowezekana kwa mila zao.
CHINA
Ukiwa China, eneo la Tibet, watibeti wegi wanaitekeleza aina hii ya ndoa hasa katika maeneo ya Tsang and Kham , lakini pia makabila mengine kama Monpa, Tamang, Qiang, Sherpa na Lhoba yakkionekana kutekeleza aina hii ya ndoa kama ilivyo kwa baadhi ya watu wa Han na Hui.
Mwanamke akiwa katika katika ndoa ya aina hii, kuna wakati halazimiki kumtaja baba wa mtoto wake ni nani kati ya waume zake. Anafanya hivyo ili kulinda mahusiano na upendo baina ya waume zake.
Utafiti mmoja uliofanywa mwaka 2008 kwenye vijiji kama Xigaze na Qamdo ulionyesha asilimia 20-50% ya familia zilikuwa za ndoa ya mwanamke mmoja aliyeolewa na wanaume wawili au zaidi. Katika baadhi ya maeno ya ndani ndani huko vijijini, idadi ya ndoa hizi ni kubwa zaidi mpaka kufikia asilimia 90%.
Lakini kwa maeneo ya mjini nchini China, ndoa ya aina hii si jambo linalopendwa na kutekelezwa na wengi, ikionekana kama jambo lisilo na maana.
NEPAL
Nepal, moja ya nchi masikini katika bara la Asia, inapatikana kwenye milima ya Himalaya. Ndoa ya mwanamke mmoja kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja zilipigwa marufuku mwaka 1963 lakini jamii katika maeneo ya Humla, Dolpa na Kosi wao wanaendeleza ndoa hizo.
Wanasema ni sehemu ya mila zao na hawawezi kuacha kirahisi, kwa msigi huo wanasema wanaheshimu zaidi mila zao kuliko sheria. Katika maeno haya, ni jamboi la kawaida na unaweza kukuta kijiji kizima kinafamilia zenye ndoa za aina hii.
Akii ndoa hii ni kitu cha kawaida pia katika baadhi ya makabilia Kaskazini na kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kama Bhote, Sherpa a Newbie.
INDIA
Kabila zaidi ya moja nchini India watu wake wanatekeleza ndoa ya aina hii. Tena China yapo makabila ambayo mwanamke anaolewa na wanaume mpaka wanne kwa wakati mmoja. Katika maeno kama Kinnaur huko Himachal kusini mwa nchi hiyo yalipo makabila ya Nilgiris, Nanjanad Vellala na Nair au Nayar, ndoa hizi ni za kawaida sana. Pia ni kawaida huko Jaunsar-Bawar kaskazini mwa India.
Katika aina hii ya ndoa nchini humu, mwanamke anakuwa na sauti kwenye kuamua jambo la familia, wanaume wanapaswa kumsikiliza na kuheshimu mawazo yake.
NIGERIA
Kwa Afrika hasa nchini Nigeria yapo baadhi ya maeneo ndoa za aina hii zinafanyika. Katika chapisho moja lililoandikwa na mwandishi Akinwale Akinyoade, ingawa si jambo la kawaida kwa jamii nyingi nchini humo, lakii katika baadhi ya makabila wanatekeleza ndoa hizo lakini kwa kificho.
Kwa mfano watu wa Irigwe Kaskazini mwa nchi hiyo, mwanamke anaolewa na wanaume wawili ama watatu na maisha yanaendelea. Ilikuwa kawaida na rasmi kwa jamii hii kwa mwanamke kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja.
Mwanamke alikuwa anakaa na mume mmoja, halafu anaamua kwenda kulala kwa waume zake wengine kwa zamu na baadae kurejea anapoishi. Akipata ujauzito watoto wote atakaa nao yeye lakini waume zake wote watawajibika kwa watoto hao.
Mwaka 1968, sheria ilipitishwa kukataza ndoa hizi, lakini kwa sababu ni mila sasa zinafanyika kwa siri.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin