Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OPEN UNIVERSITY YAWAPA SHAVU WALIMU SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Chuo Kikuu Huria Tanzania( Open University) kimesema kuwa ili kuendana na kasi ya Uchumi wa Kati na hatimaye Uchumi wa Juu ambao unahutaji wasomi wengi Chuo kimeamua kuwaendeleza walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa punguzo la ada ambapo walimu hao watatakiwa kulipa nusu ada. Hii itasaidia kuongeza walimu wengi ambao watazalisha wahitimu wakuendana na mahitaji ya Uchumi wa Kati na ule wa viwanda.

Akizungumza katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maonesho ya 16 Vyuo vya elimu ya juu yalioandaliwa na Tume ya  vyuo vikuu Tanzania (TCU),Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa chuo hicho, Dkt Mohamed Omary Maguo amesema punguzo hilo ni kwa walimu wanaotaka kujiendeleza na diploma na degree  tu.

"Ofa ambayo tunaitoa kwa sasa ni kwa walimu wa shule ya msingi na Sekondari kama unataka kujiendeleza kwa ngazi ya diploma  ama degree kuna punguzo la ada unalipa nusu kwa miaka yote utakayosoma, kuna fomu unaijaza ambayo itasainiwa na muajiriwa wako, akimaliza kuijaza na kukamilisha taratibu zote unaanza masomo",amesema Dkt Maguo. 

Sambamba na hayo, pia chuo hicho kinafundisha fani mbalimbali kuanzia ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada ya kwanza,Shahada ya Uzamili na Uzamivu, Stashahada za Uzamili na Uzamivu ambapo inategemea na mwanafunzi anataka kujiendelea katika fani ipi.

Hata hivyo, amesema, pia wana foundation program ambayo inachukua wanafunzi wa fom six waliopungukiwa na sifa za kujiunga degree pamoja na mwanafunzi wa Diploma aliepungikiwa na GPA ya kujiunga na degree.

"Pia kupitia program ya foundation inachukua mwanafunzi mwenye  NTA level 5 aliepungikiwa kujiunga na Shahada ya kwanza ambapo  wanasoma kwa muda wa miezi tisa wakimaliza wanapata fursa za kuomba  katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi"amesema Dkt Maguo.

Aidha, amesema  wanawakaribisha watanzania wote kuweza kufika katika Banda lao kwani dirisha la usajili limefunguliwa kuanzia July 26 mpaka November  mwaka huu ambapo watakua wamefunga kwa ajili ya usajili wa muhula.


Ameongeza kuwa, baada ya kupokea maombi mengi kutoka kwa watanzania mbalimbali wameweza kuongeza kozi mpya kwa mwaka wa masomo 2021/22 ya Ugavi na Ununuzi, (Procurement and supply Manegment) hivyo ni fursa kwa watu wanaotaka kusomea mambo ya biashara kuweza kuomba kozi hiyo.

Amesema kuwa, Katika kozi zote wanafunzi wanasajiliwa bure ispokua Stashahada ya Uzamili na Uzamivu ambapo mwanafunzi analipia sh elfu 30, hivyo amewaomba kutumia fursa hizo kujiendeleza kielimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com