Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), kwa Mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa Sheria ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ya 2009, Kifungu cha 6(2) ameteua Wajumbe saba (7) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Wajumbe hao walioteuliwa kwa kushauriana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban ni kama ifuatavyo:
-
- Bw. Ally Senga Gugu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara;
- Dkt. Salim Hamad Suleiman kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ);
- Bi. Vumilia Lwoga Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo;
- Bw. John Marato Sausi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango;
- Bi. Dorice John Mgetta kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA);
- Bw. Ahmed Suleiman Nassor kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA); na
- Bi. Jackline David Mkindi kutoka Taasisiya Wafanyabiashara wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA).
Uteuzi wa Wajumbe hao unaanza mara moja.
Social Plugin