Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA KUZINDUA UTOAJI CHANJO YA CORONA TANZANIA...ATACHANJWA IKULU JULAI 28


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya uzinduzi wa zoezi la uchanjaji wa chanjo ya Corona, Ikulu Jijini Dar es Salaam, Julai 28, 2021 saa 3 asubuhi ambapo Rais Samia atachanjwa.

Kupitia taarifa rasmi ya Wizara ya Afya, Dk. Gwajima amesema baada ya uzinduzi huo Wizara ya Afya itaendelea na taratibu nyingine za usambazaji wa chanjo hiyo na kutoa utaratibu wa utoaji wa chanjo katika vituo vilivyoandaliwa Mikoani.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com