Sergio Ramos (35) amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya PSG ya Paris akitokea Real Madrid ya Uhispania ambako amekaa kwa miaka 16.
Paris St-Germain imemsajili Sergio Ramos kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya mchezaji huyo kuondoka katika klabu yake ya miaka mingi Real Madrid.
Ramos , 35 aliondoka Madrid baada ya miaka 16 wakati kandarasi yake ilipokamilika mwisho wa mwezi Juni.
Akiwa klabuni hapo ameshinda mataji ya Klabu Bingwa (4), La Liga (5) na Klabu Bingwa ya Dunia (4)
Mchezaji huyo ambaye ameichezea mara nyingi zaidi timu yake ya taifa kushinda mchezaji yeyote yule ,ameshinda mataji matano ya La liga na mataji manne ya kombe la klabu bingwa akiichezea Real Madrid.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Social Plugin