WAWILI WAKAMATWA KWA MADAI YA KUMILIKI KARAKANA YA KUTENGENEZA SILAHA ZA KIENYEJI
Tuesday, July 06, 2021
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumiliki karakana ya kutengeneza silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali na kuziuza kwa wahalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga, amesema kufuatia msako uliofanyika katika Kijiji cha Chilendu, Kata na Tarafa ya Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa walikamatwa watuhumiwa hao, ambao majina hayakutajwa, wakimiliki karakana ya kutengenezea silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali.
Lyanga amesema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na gobole tano zilizo tayari, baruti gramu 408, goroli vipande vya chuma 40, fremu za silaha mbili na vifaa mbalimbali vya uchongaji wa silaha hizo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin