Dodoma- Julai 22, 2021
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mhe, Innocent Lugha Bashungwa (Mb) amewateua Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Taifa CUP, kwa ajili ya kusimamia mashindano ya mwaka 2021.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hassan Abbasi imefafanua kuwa, kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Singo Omary ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini na Makamu wake, Ameir Mohammed Makame ambaye ni Kamishna wa Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wajumbe wengine 12.
Wajumbe 12 wa Kamati hiyo ni kama wanavyoonekana hapa chini:
Bw. Shaibu Muhamed. Kamishna wa Vijana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2. Bi. Neema Msitha. Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa 3. Bw. Jackson Ndaweka. Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania 4. Bw. Michael Mwita. Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania 5. Bw. John Nguchiru. Katibu Mkuu Chama cha Michezo ya Jadi 6. Bw. Wilfred Kidao. Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 7. Bw. Leonard Thadeo. Mratibu wa Michezo, OR-TAMISEMI 8. Bw. Shaffih Dauda. Mdau wa Michezo
Bw. Mbaki Mutahaba. Mdau wa Michezo
Bw. Ally Mayai. Mdau wa Michezo
Bi. Eunice Chiume. Mwakilishi wa Benki ya NMB
Bw. William Kallaghe. Mwakilishi wa Benki ya NBC
Aidha, Waziri Bashungwa amesema mashindano hayo yatafanyika mwezi Desemba mwaka huu na yatahusisha baadhi ya michezo ya kipaumbele. Michezo ya kipaumbele inajumuisha Soka, Riadha, Ngumi, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu na Mpira wa Pete (Netiboli).
Social Plugin