WAZIRI GWAJIMA ATETA NA UONGOZI MOI, AUPONGEZA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATANZANIA
Sunday, July 18, 2021
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima jana amekutana na kufanya kikao na Uongozi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).
Dkt. Gwajima ameipongeza Taasisi ya Mifupa MOI kwa kendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kipindi cha miaka 25.
“ Hongereni mnafanya kazi nzuri, nimekuja hapa tujadiliane ili tuone ni namna gani MOI itafikisha miaka 30 ikiwa bora Zaidi, kueni huru kuchangia mada ili tusonge mbele Zaidi.” Alisema Dkt Gwajima
Amesema pamoja na huduma nzuri nafahamu kwamba Kuna changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa ili tuendelee kutoa huduma Pamoja na mambo mengine.
Dkt. Gwajima amepokea maoni, michango pamoja na changamoto mbalimbali zinazolenga kuboresha hali ya utoaji huduma katika Taasisi yaTiba na Mifupa (MOI).
Hata hivyo Dkt.Gwajima amewapa siku kumi Taasisi hiyo kuandaa taarifa watashughulikiaje changamoto zilizo ndani ya uwezo na kuziwasilisha kwake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI Prof. Charles Mkonyi amesema Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI) ina mpango wa kuanzisha kliniki katika wilaya za mkoa wa DSM ili kuwasogezea huduma Wananchi.
“Pamoja na kuanzisha hizi kliniki pia tunalenga kujenga hospitali ya kisasa ya utengamao katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Mpiji jiji Dar es. Salaam, Alisema Prof. Mkonyi.
Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema Taasisi ya MOI imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi ili kupunguzia adha ya kusafiri kufuata huduma Dar es Salaam.
“Tumesogeza huduma za kibingwa za ubongo KCMC pamoja na Bugando tumesogeza huduma za Mifupa, Hospiali ya kanda Mbeya na Nyangao Lindi Alisema Dkt. Boniface.
Dkt. Boniface amesema Maabara ya kisasa ya Ubongo (Angio Suit) iliyoanzishwa hivi karibuni tayari wagonjwa 27 wameshafanyiwa upasuaji.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin