SERIKALI KUONGEZA NGUVU KATIKA UZALISHAJI ILI KUKABILI CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA MALIGHAFI ZA VIWANDA NCHINI

Na Eliud Rwechungura
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameeleza kuwa Serikali itaongeza nguvu ya uzalishashi katika Kilimo, Mifugo, uvuvi na vyuma ili kukabili  changamoto ya upungufu malighafi inayokabili viwanda vingi nchini na kusababisha viwanda hivyo kuzalisha chini ya uwezo na kiwango cha uzalishaji.

Waziri Prof. Mkumbo ameyasema hayo Julai 03, 2021 Dar es salaam alipotembelea kiwanda cha OK Plast Ltd kinachozalisha bidhaa za nyaya za umeme Pamoja na mikeka na kukuta kuna changamoto ya upungufu wa malighafi ya mabaki ya shaba kwa ajiri ya kiwanda hicho.

“Nikili kwamba moja ya changamoto kubwa katika viwanda vya Tanzania kwa sasa ni malighafi sio idadi ya viwanda, idadi ya viwanda ipo ya kutosha lakini viwanda vyetu vingi vinazalisha chini ya uwezo kwa sababu ya kukosekana kwa malighafi kwahiyo tuna kazi kubwa ya kuongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo, uvuvi na vyuma” ameeleza Prof. Kitila Mkumbo

Aidha, Waziri Prof. Mkumbo ameeleza kuwa atakutana na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira ili kujadili na kuona namna ya kusaidia kiwanda hicho na viwanda vingine vyenye changamoto ya malighafi ya mabaki ya shaba na chuma ili kuona namna ya kusaidia mabaki hayo kuuzwa kwa viwanda vya ndani kuliko kusafilishwa kwenda nje.

Waziri Prof. Mkumbo amtumia nafasi hiyo kuwahimiza watanzania kununua bidhaa zilizozalishwa hapa nchi na zilizodhibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania maana kwa sasa viwanda vya ndani vinazalisha bidhaa bora na zenye viwango.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Sheria na Uzingatiaji Sheria wa Kiwanda cha OK Plast Ltd, Bw. Anackreto Pereilla ameishukuru Serikali kuwa kusikiza Changamoto yao ya upungufu wa malighafi ambayo imekuwa adimu kutokana na malighafi hiyo kusafirishwa kwenda nje, hivyo amewaomba mawaziri wenye dhamana kuona namna ya kuzuia malighafi hiyo kwenda nje ambayo imesababisha uzalishaji kupungua na kupelekea kupunguzwa wafanyakazi katika kiwanda hicho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post