Wachezaji wa Yanga wakishuka kwenye Ndege baada ya kufika mkoani Kigoma
Kikosi cha Yanga SC kimefika salama mkoani Kigoma tayari kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya watani zao Simba SC mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili Julai 25, 2021 katika dimba la Lake Tanganyika.
Timu hiyo ya wananchi iliondoka leo Asubuhi jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege, na wamewatangulia watani zao Simba ambao bado wapo Dar es salaam. Huu utakuwa ni mchezo wa nne timu hizi zinakutana msimu huu kwenye mashindano yote, kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu Yanga wameshinda mchezo mmoja na wametoka sare mchezo mmoja lakini pia Yanga waliifunga Simba kwenye fainali ya Mapinduzi Cup kule visiwani Zanzibar kwa mikwaju ya penati 4-3.
Na kueleka mchezo huu wa fainali tayari shirikisho la soka nchini TFF limetangaza waamuzi watakao chezesha mchezo huu, ambapo mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga kutoka Manyara, mwambuzi msaidizi namba moja yani Line 1 ni Ferdnand Chacha kutoka Mwanza, msainizi namba mbili Line 2 ni Mohamed Mkono wa Tanga na mwamuzi wa akiba yani fourth official ni Elly Sassi wa Dar es salaam.
Chanzo -