Mfanyabiashara na Mzazi mwenza wa staa wa Bongofleva na bosi wa Wasafi Media, Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari the boss lady’ ameamua kumpiga chini mpenzi wake maarufu kwa jina la King bae au Dark Stallion, baada ya kuona hana manufaa naye.
Zari ambaye anaishi Afrika Kusini pamoja na watoto wawili wa Mondi, aliandika ujumbe kwenye insta story yake,kuwa mwanaume huyo inabidi amuache kwani hana faida yoyote kwake.
“Nimemmisi, lakini inanibidi nimuache aondoke. Kwa sababu kama hanijengi, hana faida kwangu siwezi kuendelea naye,” ameandika Zari
Kufuatia hali hiyo baadhi ya mashabiki wamedai kuwa hii inaweza kuwa muda muafaka kwa Mondi kurudisha majeshi kwa Zari baada ya Dark Stallion ambaye alikuwa raia wa Nigeria kutimuliwa.
Social Plugin