Chuo kikuu Cha Zanzibar, ZANZIBAR UNIVERISTY (ZU) Cha Tanzania visiwani kimeendelea kung'ara kwenye maonyesho ya kumi na sita (16) yanayoandaliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania.
Dr .Salama Yusuf ambaye ni muadhili Mkuu wa chuo hicho wakati wa mazungumzo yake leo Julai 28,2021 amesema wanawakaribisha wanafunzi mbalimbali na wa jinsia zote kufika chuoni kwao.
Amesema kwenye maonyesho hayo wanafanya udahili na inakuwa rahisi kwa mzazi au mwanafunzi kufanyiwa udahili kwenye banda lao..
Aidha Dr. Salama aliwashauri waandaaji wa Maonyesho hayo kuyaboresha zaidi kwa sababu ni msaada mkubwa kwa wazazi ama wanafunzi,
Alisema pia (ZU)ni chuo kizuri chenye walimu wazuri na mwanafunzi akimaliza chuoni hapo anakuwa mbobezi wa suala ambalo alilisomea.
Aidha Alisema kutokana na wimbi la tatu (3)la Uviko-19 Zanzibar University inakabiliana sana kwani kuna sehemu maalumu yenye maji tiririka na sabuni
Alisema wanapokuwa sarasani wanawaweka anafunzi kwa umbali kidogo na hata mwalimu anahakikisha wanafunzi wote wamevaa barakoa