SERIKALI KUONDOA TATIZO LA AJIRA NCHINI

Na Dotto Kwilasa ,Dodoma
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Patrobas Katambi amesema ili kuondoa tatizo la ajira nchini  Serikali imewekeza nguvu  kwa kuwawezesha vijana kufanya kazi kwa kuzingatia ajira binafsi.

Katambi amesema hayo Jijini Dodoma leo Jumatano Agosti 12 ,2021  wakati akizungumza na vijana kwenye maadhimisho ya Siku ya vijana duniani na kusema kuwa serikali imeandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana wa kitanzania kujiajiri na kufikia fursa za kiuchumi.

Amesema  kwa kutambua kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa serikali imeweka utaratibu wa kuwawezesha vijana mitaji ili waweze kujiajiri ikiwa ni Pamoja na kuwatengenezea mazingira ya kukubali kujitolea kufanya kazi kabla ya ajira ili kupata uzoefu.

"Natoa wito kwa vijana kukubali kutengeneza fursa za ajira kwa kukubali kujitolea kwenye mashirika na Taasisi ambazo zinahusiana na taaluma zenu,hii itasaidia kuwapa ujuzi na kuwa na nafasi nzuri pindi ajira zinapotokea,"amesema.

Kutokana na hayo Mwakilishi wa Tanzania Communications Analyst (UNFPA) Dk.Mariam Ngaenje wakati akiwasisha ujumbe wa UNFPA kwenye maadhimisho hayo amesema kuwa zaidi ya vijana 1.8 bilioni wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanaishi katika nchi zinazoendelea na nusu yao wanafanya kazi katika sekta ya kilimo na chakula.

Ameeleza kuwa hali hiyo inatokana na Takwimu zinazoonyesha kwamba kuna vijana bilioni 1.2 duniani wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 duniani kote kati ya hao milioni 207 sawa na asilimia 17.3 wanakabiliwa na tatizo la uzito uliokithiri.

"Vijana milioni 207 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 duniani kote wanasumbuliwa na tatizo la uzito uliokithiri.ali na hayo watoto wa kike wapo katika hatari zaidi ya kupata utapia mlo na hadhari za mila na desturi ambazo usababisha ukosekanaji wa vyakula vyenye virutubisho,elimu bora na fursa za Kiuchumi.

"Hivyo mifumo imara ya uzalishaji wa chakula ni muhimu ili kutoa fursa kwa vijana hususani watoto wa kike waweze kupata virutubisho vyote kwa njia rahisi,salama na ya kudumu"amesema Dk.Ngaeje.

Dk. Ngaeje amesema kuwa UNFPA imedhamiria kusaidia vijana na taasisi zao kama ilivyobainishwa vizuri katika mkakati wa UNFPA wa vijana unaoitwa "My Body ,My life,My World".

"Tumedhamiria kuwa kila kijana atapata elimu na taarifa sahihi,atapata huduma na anakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi juu ya mwili na maisha yake na pia anapata nafasi ya kushiriki katika mipango na utekelezaji wa program za vijana ili kuleta mabadiliko katika jamii", ameeleza Dk.Ngaeje.

Naye Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shirika la Action Girls Foundation, Rabia Saada wamekuwa na mazimio na kati ya maazimio ni pamoja na kuiomba serikali kuharakisha mchakato wa uharakishwaji wa mchakato mzima wa baraza vijana.

"Tumeiomba serikali kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana,kuwapa nafasi za Maamuzi na kuwajengea uwezo pamoja na Wizara husika kutoa tadhimini ya mapendekezo ya vijana yanayotolewa kila mwaka"ameeleza Rabia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post