Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA HILAL AOMBOLEZA KIFO CHA ELIAS KWANDIKWA..... "HATA NILIPOKOSA UBUNGE HUKUNIACHA"

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (katikati kwenye picha)  ameomboza kifo cha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandikwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga aliyefariki dunia Jumatatu saa 2 usiku Agosti 2,2021 wakati akiendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Eligaesha amesema kuwa Waziri Kwandikwa alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo kwa takribani wiki mbili.

Kufuatia kifo hicho, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad amesema Kwandikwa ameacha alama katika utumishi wake na kwamba Mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla limepoteza mtu muhimu.

"Hakika kila nafsi itaonja mauti; Pumzika kwa Amani Kiongozi,Kaka na Rafiki wa wengi Mh Elias Kwandikwa, Hakika ulikuwa na Upendo mkubwa sana Sitakusahau katika suala la Maendeleo ndani ya jimbo la Ushetu na Mkoa wa Shinyanga. Ulikuwa na Upendo na Huruma kwa wengine, ulikuwa msaada mkubwa kwangu kwenye siasa na maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga, mara kwa mara tulijadiliana na kushauriana tufanye nini", amesema Azza.

"Hata nilipokosa Ubunge hukuniacha,hakika ulikuwa Rafiki wa kweli na siyo kwa sababu ya madaraka. Pole nyingi kwa Familia, Wananchi wa Jimbo la Ushetu na Mkoa mzima wa Shinyanga.
Umeacha alama katika Utumishi wako,hakika Shinyanga tumeondokewa.
Mwenyezi Mungu Akupe Pumziko la Amani. 😭😭", amesema Azza.


Soma pia :
RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI ELIAS KWANDIKWA

Tanzia : WAZIRI WA ULINZI NA JKT - MBUNGE WA USHETU ELIAS KWANDIKWA AFARIKI DUNIA

Hapa chini ni baadhi ya picha Azza Hilal wakati huo akiwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga akiwa na Elias Kwandikwa kwenye matukio mbalimbali.
Aliyesimama ni Elias Kwandikwa enzi za uhai wake



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com